Grace Mugabe, Mke wa Rais wa zamani wa Zambia, Robert Mugabe

Polisi Afrika Kusini wamsaka mke wa Mugabe

MAMLAKA ya Taifa ya Mashtaka nchini Afrika Kusini (NPA) imetoa hati ya kukamatwa kwa Grace Mugabe, mke wa Rais mstaafu wa taifa hilo, Robert Mugabe kuhusiana na tuhuma zinazomkabili za kumshambulia mwanamitindo Gabriella Engels. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Afrika Kusini, Brigedia Vishnu Naidoo amethibitisha kuhusu taarifa hizo akisema kuwa, hati hiyo ilitolewa tarehe 13 Desemba 2018.

Hatua hiyo imekuja baada ya mahakama kumfutia kinga ya kidiplomasia Grace mwezi Julai mwaka huu.

Grace anadaiwa kufanya shambulizi hilo mwaka jana katika hoteli moja ya kifahali inayofahamika kwa jina la Sandton iliyopo mjini Johannesburg, ambapo mwanamitindo huyo anadaiwa alikwenda kuwatembelea vijana wa Mugabe.

Baada ya mwanamitindo huyo kutoa tuhuma hizo, Jeshi la Polisi Afrika Kusini lilimtaka Grace kufika katika kituo cha polisi, lakini hakutokea licha ya awali kuahidi kwamba angeitikia wito. Na kurejea nchini kwake Zimbabwe.

MAMLAKA ya Taifa ya Mashtaka nchini Afrika Kusini (NPA) imetoa hati ya kukamatwa kwa Grace Mugabe, mke wa Rais mstaafu wa taifa hilo, Robert Mugabe kuhusiana na tuhuma zinazomkabili za kumshambulia mwanamitindo Gabriella Engels. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea). Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Afrika Kusini, Brigedia Vishnu Naidoo amethibitisha kuhusu taarifa hizo akisema kuwa, hati hiyo ilitolewa tarehe 13 Desemba 2018. Hatua hiyo imekuja baada ya mahakama kumfutia kinga ya kidiplomasia Grace mwezi Julai mwaka huu. Grace anadaiwa kufanya shambulizi hilo mwaka jana katika hoteli moja ya kifahali inayofahamika kwa jina la Sandton iliyopo mjini Johannesburg, ambapo…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

error: Content is protected !!
Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On YoutubeVisit Us On Instagram