September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli amtolea nje Mnyika

Rais John Magufuli

Spread the love

RAIS John Magufuli amemgomea John Mnyika, Mbunge wa Kibamba na Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo kuhusu ombi lao la kuitaka serikali kuwalipa fidia wakazi wa Kimara na Mbezi waliobomolewa nyumba ili kupisha mradi wa barabara ya njia nane kutoka Kimara hadi Kibaha. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Akizungumza katika uwekaji wa jiwe la msingi katika barabara ya Kimara leo tarehe 19 Desemba 2018. Rais Magufuli amesisitiza kwamba serikali haitalipa fidia kwa watu waliobomolewa nyumba zao kupisha upanuzi wa barabara hiyo, kwa kuwa walijenga ndani ya hifadhi ya barabara.

Awali, mbele ya Rais Magufuli wabunge hao walipewa nafasi ya kutoa neno la salamu na kutumia nafasi hiyo kukumbushia machungu ya wananchi wa maeneo hayo walibomolewa nyumba zao bila ya kulipwa fidia.

“Kwa niaba ya wananchi tunashukuru kwamba umeamua kodi za walipa kodi za watanzia zitumike kujenga barabara ya njia nane …lakini ni vizuri ninapo salimia nikafikisha salamu kwa niaba ya wananchi waliokuwa pembeni wanaomba mheshimiwa rais kama vile ambavyo ulivyoomba kule Arumeru na naamini watanzaia wamekuambia kwamba usiwe na kiburi wananchi wale bado wana malalamiko juu ya bomobomoa katika eneo hili.”

“Ninakuomba mheshimiwa rais kwa kutanguliza utu mbele Mwalimu Nyerere alisema maendeleo ni ya vitu na watu lakini maendeleo zaidi ni ya watu pamoja na ujenzi wa njia nane utafakari vilevile kuwalipa fidia waliobomolewa kupisha ujenzi wa barabara hii ya njia nane” amesema Mnyika.

Amesema kuwa Demokrasia na Maendeleo ni vitu vinavyoambatana na vinavyotegemea “Demokrasia na Maendeleo ni mapacha tunakuomba mheshimiwa Rais unapofanya kazi za miradi ya maendeleo vilevile ukatumia fursa hiyo kuondoa vikwazo vinavyoikabili Demokrasia ambayo tunamini itasaidi kwa nchi kusonga kasi zaidi kimaendeleo.”

Wakati huo huo amemueleza Rais kuwa ana ujumbe wenye hoja tano kutoka kwa Mwenyekiiti wa Chadema Freeman Mbowe aliyepo Mahabusu ya Magereza ya Keko kutokana na kufutiwa dhamana kwenye kesi inayomkabili yeye na viongozi wengine waandamizi wa chama hicho.

Kubenea akipigia msumali suala la bomoabomoa ameleza kuwa wananchi wa maeneo hayo wana kinyongo kutokana na kutoliwa fidia ya kumolewa kwa makazi yao.

Kubenea amemtaka Rais kudumisha Demokrasia nchini ambayo itakuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi nchini.

error: Content is protected !!