Saturday , 11 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Mu-Iran aliyewapa taarifa CIA, Israel kunyongwa
Kimataifa

Mu-Iran aliyewapa taarifa CIA, Israel kunyongwa

Mahmoud Mousavi-Majd
Spread the love

MAHMOUD Mousavi-Majd, Raia wa Iran aliyesaidia Intelejensia ya Marekani (CIA) kumuua kamanda wa ngazi ya juu wa Iran, Qassem Soleimani amehukumiwa kunyongwa hadi kufa. Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).

Januari 3 mwaka huu, ndege zisizo na rubani za Marekani nchini Iraq, zilimuua Kamanda Soleimani. Serikali ya Washington ilimlaumu Soleimani kwamba ndiye aliyekuwa akipanga mashambulizi kwenye kambi zake katika ardhi ya Iraq.

“Mahmoud Mousavi-Majd, mmoja kati ya watu walioisaidia the CIA, amekutwa na hatia na amehukumiwa kunyongwa mpaka kufa. Huyu ndio alikokuwa akiwapa taarifa maadui zetu kuhusu kamanda Soleimani.

“Majd aliwapa taarifa intelejensia ya Israel na Marekani taarifa zote za jeshi la Iran.” amesema Gholamhossein Esmaili, msemaji wa mahakama kuu nchini humo na kwamba, Majd’s atanyongwa katika siku za karibuni

Hata hivyo, taarifa ya baadaye iliyotolewa na mahakama hiyo ilidai kwamba, kunyongwa kwa Majd hakuna uhusiano na ushirikiano wake na CIA.

“Kesi kuhusu tuhuma za ukuwadi zilianza kabla ya kuuawa kwa Soleimani,” taarifa ya mahakama ilieleza hivyo. Majd alikamatwa Oktoba 2018.

Mwaka 209, Iran ilitangaza kwamba, kuna maofisa wake 17 wamekuwa wakifanya kazi na CIA, na kueleza miongoni mwao watanyongwa.

Kuuawa kwa Soleimani kulieleza kufikia kilele cha mgogoro kati ya Marekani na Iran. Iran iliamua kushambulia kambi za Marekani zilizokuwepo Iraq.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

KimataifaMakala & Uchambuzi

Mbivu, mbichi urais wa Ramaphosa mwezi huu

Spread the loveMWISHONI mwa mwezi huu, raia wa Afrika Kusini watapiga kura...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

error: Content is protected !!