Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa ‘Hiki ndio kilio kikuu cha Wapalestina’
Kimataifa

‘Hiki ndio kilio kikuu cha Wapalestina’

Spread the love

PALESTINA haihitaji kupendelewa, kubebwa wala kubembelezwa bali inahitaji haki yake na hiki ndio itasimamia milele. Anaripoti Yusuph Katimba … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 21 Februari 2019 Hamdi Mansour AbuAli, Balozi wa Palestina nchini Tanzania amesema, dunia inajua kuwa, Wapalestina wanapambana kuhakikisha wanabaki na kile kilicho stahili yao na si vinginevyo.

Balozi AbuAli ametamka kauli hiyo baada ya maelezo ya awali kutokana Dk. Uri Davis, Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi Palestina.

Katika mkutano huo Dk. Davis amesema, tatizo kubwa ni uvamizi wa makazi unaofanywa na Israel dhidi ya Plestina huku Marekani ikiwa na mchango mkubwa kwenye uvamizi huo.

Amefafanua kuwa, kinachofanywa na Israel dhidi ya Palestina hakina tofauti na kile kilichokuwa kikifanywa na Makaburu wa Afrika Kusini kwa wenyeji wa taifa hilo.

“Tofauti yake ni kuwa, Afrika Kusini ukandamizaje wake uliisha wakati ukandamizaji wa Israel dhidi ya Wapalestina unakuwa siku hadi siku,” amesema Dk. Davis.

Mwanaharakati huyo aliyezaliwa katika Mji wa Jerusalem miaka 75 iliyopita amesema, ndani ya Plestina hakuna mtu hata mmoja aliyetaka kubeba bomu na kwenda kuwalipua Waisrael.

“Hakuna mtu anayebeba bomu na kwenda kuipua kwa Waisrael, hakuna bali Israel ndiyo inayokwenda kwenye ardhi ya Wapalestina na kutekeleza uvamizi. Mamilioni ya Wapalestina tayari wamefukuzwa kwenye makazi yao,” amesema.

Hata hivyo Balozi AbuAli amesema, kinachofanyika Palestina kinawaumiza watu wa dini na rangi zote kwa kuwa, Palestina wakazi wake ni Waislam, Wakristo, Wajahudi na makundi mengine.

“Ukandaamizaji unaofanywa na Israel katika ardhi ya Wapalestina unaumiza dini na makabila yote. Rais wa Palestina ni Waislam, Wakristo, Wayahudi na madhehebu mengine,” amesema Balozi AbuAli na kuongeza;

“Palestina inapigania uhuru wake ambao ni haki yake ya msingi. Inapigania ardhi yake na si kuwa, inahitaji kupendelewa. Hatuwezi kulazimishwa kupokea mawazo ya wengine katika nchi yetu.”

Balozi AbuAli ameishukuru Tanzania kuwa kuitambua Palestina na kutoa ushirikiano wake katika mambo mbalimbali ikiwepo katika sekta ya utalii. Mwaka jana Palestina iliingia kwenye makubaliano ya masuala ya Utalii na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Tarehe 11 Oktoba 2018 Balozi AbuAli alipozungumza na vyombo vya habari alisema, “Wapalestina wanataabika kutokana na Israel kuondoa furaha yetu. Juhudi za kutatua mgogoro zinashindikana kufikiwa kutokana na Israel kushindwa kuheshimu makubaliano ya Umoja wa Mataifa (UN),” amesema AbuAli akisitiza Palestina itaendelea kupigania utambulisho wake.

Alisema, yapo mambo yanayoonesha kuwa, wanaosimamia mazungumzo ya muafaka hawalengi kupata muafaka wa mgogoro wa Palestina na Israel kwa sababu ya kuubeba upande mmoja na kisha kuukandamiza upande mwingine.

“Angalia namna Marekani ambaye ndio msuluhishi, anachukua ardhi ya Wapalestina (Jerusalem) na kuwakabidhi Israel halafu hapo hapo anakwita kwenye meza ya mazungumzo. Unawezaje kumwamini mtu wa namna hii?” amehoji AbuAli.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!