Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Zungu alia popo kukithiri Kivukoni
Habari Mchanganyiko

Zungu alia popo kukithiri Kivukoni

Spread the love

 

NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Azan Zungu, ameitaka Serikali kuchukua hatua za haraka kuondoa popo wanaoharibu mazingira maeneo ya Kivukoni, jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Zungu ametoa wito huo katika kipindi cha maswali na majibu, leo Jumatano, bungeni jijini Dodoma.

“Kuna kero ya popo katika Kata ya Kivukoni, hawa waharibifu wanachafua mazingira wananchi wanalalamika. Hatua gani mnachukua kuondoa popo Kivukoni?” amehoji Zungu.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Marry Masanja, amesema mbinu mbadala za kuwaondoa wanyama hao zinatafutwa baada ya mbinu za awali zilizofanyika kutozaa matunda kwa kuwa wanaondolewa kisha baada ya muda wanarejea.

“Ni kweli kuna changamoto, popo wamezunguka maeneo ya Dar es Salaam hususan yanayozunguka Ikulu. Serikali imeanza kufanya kazi, tumewahi kuwapunguza lakini changamoto tunapowaondoa wanaondoka ikifika muda wanarudi. Tumefanya utaratibu wa kutafuta mbinu mbadala,” amesema Masanja.

1 Comment

  • Orodha ya Harufu ZINAZOsababisha magonjwa:- a + b(Harufu ya Kinywa/MAFUTA) +c(Harufu ya kuTAKATAKA) +d(Harufu ya Bia/SIGARA/CHAKULA) +e(Harufu ya Kwapa/HELA) +Error Term(PAMBANA nazo DAIMA KAZI TOSHA)

    Nani apewe Mungu kwenye Ulimwengu wa Utandawazi (Views Analysis – Tukang’oe SGR hatuna hadhi nayo):- a + b (26,130,474 – I miss you) + c(3,811,526 – Nandy – Siwezi) + d(633- Bunge la 12) + Error Term

    Ulijua waTANZANIA wanaishi vizuri (HUTAKIWI KUBORESHA KITU) ulivyokunywa bia GANI:- a + b(Flying Fish) + c(Safari) + d(Kilimanjaro) + f(Bingwa) +g(Four cousins) + h(RITZ) + i(Serengeti) + Error Term

    Sura GANI inatakiwa kumiliki NYUMBA/GARI(Dummy Variable, 0-Kumiliki 1-Kutokumiliki): a + b(Sura ya Abdul) + c(Sura ya Jesca) + d(Sura ya January) + g(Sura ya John) + h(Sura ya Grace) + j(hamo) +Error Term

    UNUNUZI WA GARI UPI HAUNA USUMBUFU:- a + b(yard) + c(be forward) + d(used car ya tanzania) + e(Gari ya Baba/Mjomba/Shangazi/Baba mdogo/ Mama mdogo/ Kaka au ndugu kwa ujumla) + Error Term

    Used 2014 BMW MINI COOPER CROSSOVER ALL 4/DBA-XD16 for Sale BN455840 – BE FORWARD

    Kodi ya VAT INAVYOJENGA TAIFA indirect:- Mfanyakazi kapewa mshahara wa 200,000 atasaidia kujenga nyumba za watu wafuatao.. BAR (NYUMBA 1), CHAKUA (NYUMBA 1), SIGARA/BIA(NYUMBA 7), VOCHA (NYUMBA 1), HARDWARE(NYUMBA 1), VOCHA (NYUMBA 1), MAFUNDI (NYUMBA 2)… – NCHI YA AMANI HIYOO

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!