JESHI la Polisi Mkoani Tabora limewanasa watu 21 kwa tuhuma ya kujihusisha na wizi wa vifaa vya na miundombinu ya maji mali ya Mamlaka ya maji Safi na Usafi wa Mazingira mkoani Tabora (TUWASA). Anaripoti Paul Kayanda, Tabora … (endelea).
Akizungumza jana tarehe 19 Aprili 2023 na waandishi wa habari mkoani Tabora. Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Richard Abwao amesema hatua hiyo imefanikishwa na kikosi kazi cha wilaya ya Tabora kilichoundwa kwa kushirikisha askari polisi na watumishi TUWASA.
Pia amesema katika operesheni hiyo, askari walikamata vitu vilivyoibiwa ambavyo ni pamoja na nondo 353, connector mbili, koki 43, gate valve 11, stand za mita ya maji mbili, vipande vya bomba3/4 21, valve handle moja, vipande vya bomba za barabarani 12, binding wire moja, bomba 33, mizani ndogo moja, bati tatu na vitanda viwili vya chuma vya friji za mochwari.
Ameongeza kuwa baada ya upelelezi kukamilika watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma zinazowakabili.
Leave a comment