May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga, Simba kuweka kambi Morocco

Spread the love

 

TIMU kongwe nchini Tanzania za Simba na Yanga zote za jijini Dar es Salaam, zinatarajia kukwea pipa kwenda nchini Morocco kwa ajili ya kuweka kambi ya maandalizi ya msimu ujao wa 2021/22. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Simba ambao ni mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara kwa misimu minne mfululizo pamoja na mabingwa wa kombe la shirikisho kwa misimu miwili mfululizo wamesema watakwenda kuweka kambi Morocco.

Tizo zote mbili ambazo zimekuwa katika pilika pilika za usajili kwa ajili ya kujiimalisha na msimu ujao wa mashindano 2021/22, zimetumia kurasa zao za kijamii kuelezea maandalizi ya kambi zao.

Leo Jumanne, tarehe 10 Agosti 2021, Simba imeweka taarifa ya maandalizi ya kambi hiyo na kusema “𝗠𝗼𝗿𝗼𝗰𝗰𝗼 ndio nchi ambayo mabingwa wa nchi tutaweka kambi kujiandaa na msimu mpya wa 2021/22.”

Wakati watani zao Simba wakisema hivyo, wao Yanga wanaotoka mitaa ya Jangwani na Twiga wamesema “kikosi cha timu ya Wananchi kitaondoka Dar es Salaam kwenda Morocco kwa maandalizi ya msimu ujao.”

Watani hao wa jadi, ndio watakaocheza mechi ya Ngao ya Jamii tarehe 25 Septemba 2021, katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, kuashiria ufunguzi wa msimu ujao wa mashindano 2021/22.

error: Content is protected !!