Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Tangulizi Wadau wataja muarobaini ukatili wa kingono vyumba vya habari
Tangulizi

Wadau wataja muarobaini ukatili wa kingono vyumba vya habari

Dk. Ayubu Rioba, mkurugenzi Shirika la Habari TBC
Spread the love

 

VYOMBO vya Habari nchini Tanzania, vimetakiwa kufuata miongozo na sera zilizowekwa na Serikali na taasisi binafsi, kwa ajili ya kudhibiti vitendo vya ukatili wa kijinsia, hasa ukatili wa kingono kwa wanawake.Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Wito huo umetolewa leo Jumanne, tarehe 10 Agosti 2021, katika mjadala wa kujadili sera za kuzuia unyanyasaji wa kijinsia katika vyumba vya habari, ulioendeshwa na Taasisi Internews, kwa kushirkiana na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF).

Akizungumza katika mjadala huo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dk. Ayub Rioba,amesema ili ukatili wa kijinsia utokomezwe, vyombo vya habari hasa vya watu binafsi, vinatakiwa kuanzisha sera za kijinsia pamoja na kuzingatia usawa wa kijinsia.

“Endapo wizara na asasi zote pamoja na waajiri wote, wangekuwa na sera ya aina hiyo pahala pa kazi na kuwa na muongozo huo, lengo ikiwa kupinga unyanyasaji wa aina yoyote, ubaguzi na unyanyasaji wa kijinsia hautakuwepo,” amesema Dk. Rioba.

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake nchini Tanzania (TAMWA), Joyce Shebe, amesema ili changamoto hiyo iishe, inatakiwa iwepo mifumo imara ya kudhibiti vitendo vya ukatili wa kijinsia.

“Kutokuwepo mifumo ya kuzuia ukatili ni changamoto, vyombo vingi havina hiyo sera na kama zipo ni kwa media chache sana na hao walionazo ukiulizia itakuwa nusu au robo tatu ya wafanyakazi, hawaijui hiyo sera. Lakini uelewa kwa sera husika, tuna changamoto kubwa ya uwepo wa hiyo mifumo, hivyo inaongeza ukubwa wa tatizo,” amesema Shebe.

Absalom Kibanda amesema, changamoto hiyo haijaanzia ndani ya vyombo vya habari, bali katika jamii, hivyo ili imalizwe inapaswa jitihada kubwa zielekezwe katika jamii kwa ujumla.

“Ili tuondoe, lazima tutatue tatizo hili kwenye jamii, hatuwezi kumaliza ndani ya vyumba vya habari kama jamii ina ukatili wa kijinsia. Tufanye nini? Wakati tunahimiza usawa wa kijinsia, vita hii ielekezwe nje ya vyumba vya habari, ikifanywa na wahariri na waandishi. Tukifanya hivyo tutachagiza vita hii nje,” amesema Kibanda.

Naye Tausi Mbowe, amesema ili tatizo hilo liishe, inatakiwa wahanga wasikae kimya, bali wapaze sauti zao kufichua maovu hayo, ili hatua madhubuti zichukuliwe.

“Tatizo kubwa ni kuchukua hatua, mambo haya tunayaona ya kawaida sana, inatia aibu lakini kwenye vyumba vya habari tunaona ya kawaida, kushikwa mtu inakuwa kawaida, tunaona vitu vya kawaida, takwimu za matukio hayo ni mbaya,” amesema Mbowe.

Abdallah Majura, ameshauri vyombo vya habari vifunge kamera maalum (CCTV Camera), kwa ajili ya kuona watu wanaohusika na vitendo hivyo.

“Vyombo vya habari vitekeleze hizo sera kwa vitendo na visiishie kuweka kabatini , vyumba vya habari wafunge CCTV kamera, wakamate wanaofanya vitendo hivyo,” amesema Majura na kuongeza:

“Lakini ulipaji watu uwe mzuri, usipolipa vizuri watu wanachukua nafasi hiyo kufanya vitendo vyao na mtu mwenye ujinga ule aripotiwe ili asipate kazi katika chombo chochote.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Vigogo wanaokwamisha mradi Liganga na Mchuchuma kitanzani

Spread the love  NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Zungu, watu wanaokwamisha utekelezaji...

Habari MchanganyikoTangulizi

Hii hapa kauli ya Sheikh mpya mkoa wa Dar

Spread the loveSAA chache baada ya kuteuliwa kukaimu nafasi ya aliyekuwa Sheikh...

Habari MchanganyikoTangulizi

Breaking news! Mufti amng’oa Sheikh mkoa Dar

Spread the loveBARAZA la Ulamaa la Bakwata katika kikao kilichofanyika tarehe 1...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yatoa tamko bungeni sakatala la viboko shuleni

Spread the love  SERIKALI imewaagiza maafisa elimu wa mikoa na wilaya kuratibu...

error: Content is protected !!