Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wizara ya Madini yaja na programu ya kuinua wachimbaji vijana, akina mama
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Madini yaja na programu ya kuinua wachimbaji vijana, akina mama

Spread the love

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema Serikali itatekeleza programu ya Mining for a Brighter (MBT) kwa lengo la kuwainua wachimbaji wanawake na vijana. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mavunde ameyasema hayo leo tarehe 8 Aprili 2024 Jijini Dodoma alipokuwa akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyanyakazi wa Wizara na Taasisi zake na kutumia fursa hiyo kuwataka viongozi na watumishi wa wizara kuwa wabunifu kila wakati wanapotekeleza majukumu yao.

“Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuiimarisha wizara ya madini kwa kuitengea fedha za kutekeleza miradi na mipango mbalimbali,” amesema Mavunde.

Amesema Mpango mahsusi ambao wizara inakuja nao sasa ni kuwaendeleza wachimbaji akinamama na Vijana Kupitia programu ya Mining for A Brighter Tomorrow (MBT) yenye lengo la kuwapatia leseni za maeneo ya uchimbaji, magari, vifaa na mitambo ya uchimbaji.

Amesema kupitia programu hiyo itasaidia kuchochea ukuaji wa sekta ya madini, uchumi wa Taifa na kuongeza ajira kwa watanzania.

“Tumieni hili baraza la wafanyakazi kuhakikisha mnakuja na mpango mzuri wa kusimamia utekelezaji wa mipango na miradi chini ya Wizara,” amesisitiza Mavunde.

Aidha, ametumia fursa hiyo kuwapongeza watumishi wa wizara kwa jitihada za ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali na kueleza kuwa ana imani kubwa kwa watumishi wa wizara kuwezesha sekta ya madini kufikia mchango wa asilimia 10 kwenye pato la Taifa ifikapo 2025.

Awali, akimkaribisha Waziri wa Madini, Dk. Steven Kiruswa, Naibu Waziri wa Madini amewapongeza watumishi wote wa Wizara kwa namna wanavyoendelea kujitolea kuhakikisha mikakati yote ya kuendeleza Sekta ya Madini inafanikiwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!