Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wella asisitiza ushirikiano Same
Habari Mchanganyiko

Wella asisitiza ushirikiano Same

Spread the love

KATIBU Tawala wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Upendo Wella amewaomba viongozi, watumishi wa umma, binafsi na wananchi wilayani humo  kuendeleza ushirikiano na  uwajibikaji ili kufanikisha adhma ya kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali yake kuleta maendeleo.  Anaripoti Mwandishi Wetu, Same … (endelea).

Wella ameyasema hayo wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya ofisi baina yake na aliyekuwa Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Sospeter Magonera aliyehamishiwa Wilaya ya Hai mkoa humo katika mabadiliko ya hivi karibuni yaliyofanywa na Rais Samia.

Katibu huyo alisema ushirikiano kwenye utendaji ndio njia pekee na rahisi kwa kila mmoja kufanikisha wajibu wake, hivyo atasikitika kuona baadhi ya watoaji wa umma wanakuwa chanzo cha kudorora.

“Kazi yetu kubwa ni kuwahudumia wananchi wa Same hasa kutatua migogoro ya wenyewe kwa wenyewe na wote tuwe kitu kimoja, ili  tuendelee kukuza uchumi wa Taifa letu,” alisema Wella.

Kwa upande wake Katibu Tawala aliyehamishwa, Magonera amewashukuru watumishi na wakazi wote wa Same kwa ushirikiano katika kipindi chote cha utumushi wake kwenye wilaya hiyo, akisema kwa kua lengo la Serikali ni kujenga nchi na kuleta maendeleo, ushirikiano ndio msingi wa kufanikisha mipango hiyo.

“Nashukuru sana kwa ushirikiano wenu nyie watumishi na wananchi kwani mmenifanya nifanye kazi yangu katika mazingira mazuri, naomba muendelee na moyo huo, ili dhamira ya Rais Samia kuwaletea maendeleo iweze kutekelezeka,”alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

error: Content is protected !!