Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Tanzania yawakaribisha wawekezaji kutoka Urusi
Habari za Siasa

Tanzania yawakaribisha wawekezaji kutoka Urusi

Spread the love

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imewakaribisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Serikali ya Urusi kuwekeza nchini kwa maslahi ya pande zote mbili na ustawi wa dunia kwa ujumla. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Mwaliko huo umetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk aliposhiriki katika maadhimisho ya Siku ya Kitaifa ya Urusi jana tarehe 15 Juni 2023 Jijini Dar es Salaam.


“Tanzania ina mazingira tulivu ya biashara na uwekezaji yanayotoa fursa za uwekezaji, hivyo natoa rai wa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Urusi kuja kuwekeza Tanzania ili kuimarisha zaidi biashara baina ya nchi zetu mbili,” alisema Balozi Mbarouk

Balozi Mbarouk aliongeza kuwa Tanzania kwa kushirikiana na sekta binafsi zimeboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ili kuhakikisha kuwa uwekezaji unafanyika katika mazingira rafiki na salama na kuwafanya wafanyabiashara kutoka nje kufanya biashara zao katika mazingira salama na rafiki.


Balozi Mbarouk aliongeza kuwa Urusi imekuwa mshirika wa maendeleo ya kijamii, kiuchumi, kiteknolojia na kisiasa nchini Tanzania. Kwa kusainiwa kwa mkataba wa kuanzisha Tume ya Pamoja ya Kiserikali ya Biashara na Ushirikiano wa Kiuchumi, nchi hizo mbili zipo katika nafasi nzuri zaidi ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara na uwekezaji kwa manufaa ya pande zote mbili.

Kwa upande wake Balozi wa Urusi nchini, Andrey Avetisyan alisema kuwa ushirikiano wa Urusi na Tanzania ni wa kihistoria na umekuwa imara wakati wote. Urusi itaeendelea kushirikiana na Tanzania kijamii, kisiasa na kiuchumi wakati wote.

“Tunapoadhimisha siku hii muhimu tunakumbuka pia miaka 62 ya uhusiano kati ya Urusi na Tanzania. Aidha, Balozi Avetisyan aliongeza kuwa Urusi itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kukuza na kuendeleza ushirikiano wa kufanya kazi kwa pamoja kwa maslahi ya pande zote mbili,” alisema Balozi Avetisyan.

“Urusi itaendelea kushirikiana na Tanzania kuboresha biashara na uwekezaji ambapo kwa sasa ukuaji wa biashara baina ya mataifa yetu umeongezeka. Tunaendelea kuboresha biashara licha ya changamoto zinazojitokeza,” aliongeza Balozi Avetisyan.

Tanzania na Urusi zinashirikiana katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ulinzi, afya, biashara, viwanda, uwekezaji na utalii ambapo kwa pamoja zimekubaliana kuendeleza ushirikiano huo ili kuleta tija katika utekelezaji wa diplomasia ya uchumi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mpina mwiba CCM, ahofia kuzibwa mdomo

Spread the loveWAKATI Chama cha Mapinduzi (CCM), kikijinasibu kuwa kinara wa demokrasia...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mabeyo ametuepusha

Spread the loveNIMEGUSWA na uadilifu, utiifu na uaminifu wa Mkuu mstaafu wa...

Habari za SiasaTangulizi

CCM yaitaka TAKUKURU kuichunguza Chadema tuhuma alizoibua Lissu

Spread the loveCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana...

error: Content is protected !!