Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Waziri aeleza sababu BoT kukwama kununua dhahabu
Habari Mchanganyiko

Waziri aeleza sababu BoT kukwama kununua dhahabu

Spread the love

WAZIRI wa Madini, Dk. Doto Biteko, amesema Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imekwama kununua dhahabu kutokana na viwanda vya uchenjuaji madini nchini kutoanza kufanya kazi.

Amesema kusuasua kuanza kazi kwa viwanda hivyo, kunaifanya dhahabu inayozalishwa nchini kukosa ithibati za kimataifa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Biteko ametaja sababu hiyo leo Jumatano, tarehe 10 Machi 2022, jijini Dodoma, akielezea mafanikio ya mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassa.

Dk. Biteko ametoa ufafanuzi huo alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa sheria ya madini iliyofanyiwa marekebisho 2017.

Amesema BoT haiwezi kununua dhahabu ambayo haijasafishwa na kukidhi viwango vya kimataifa, ndiyo maana Serikali ilitafuta wawekezaji wa kujenga viwanda vya uchenjuaji, ambapo kwa sasa viko vitatu mwenye mikoa ya Mwanza, Geita na Dodoma.

“Ili ziweze kufanya kazi kuna taratibu za vibali mbalimbali vya kimataifa, vya kukuruhusu kusafisha. Wanakamilisha ithibati kwa maana mtu mwingine anaweza sema mbona viwanda vya uchenjuaji zipo lakini haijaanza, tunakamilisha taratibu za ithibati,”

Biteko amesema “ili waweze kutambua kimataifa, sababu ukichenjua bila ithibati madini yako ukiyasafisha hakuna atakayeyatambua. Utakuwa unacheza mchezo wa kuigiza, kwa hiyo hatua ya kwanza unajenga, unatafuta kibali, ukishapata dhahabu yoyote utakayoisafisha inatambuliwa kimataifa na unaweza kuiweka benki kama currency.”

Biteko amesema, viwanda hivyo vinakamilisha taratibu za ithibati ili vianze kufanya kazi ya uchenjuaji madini.

“Sasa baada ya uwepo wa refinery (usafishaji) hizo, sasa BoT hatakuwa na sababu nyingine za kununua dhahabu. Nia yetu nikwamba wanakamilisha taratibu zaoza ndani na tumekuwa tukikumbushana nao na wao wako tayari kununua,” amesema Biteko.

Wakati huo huo, Biteko amesema katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Samia madarakani, Serikali yake imeendelea kudhibiti utoroshwaji madini, kwa kuweka mikakati mbalimbali, ikiwemo ya kuondoa urasimu kwenye utoaji vibali.

“Vitendo hivyo sitaki kusema vimeisha, ila bila shaka yoyote naweza kusema vimepungua kwa kiasi kikubwa na waliopunguza ni wachimbaji wenyewe hawaoni sababu ya kutorosha madini kupeleka nje ya nchi bila kuyalipia kodi,” amesema Biteko.

1 Comment

  • Duh!
    Kwanini hakuna tarehe ya kuanza?
    Au vinahujumiwa visianze kazi?
    Mama, naomba viongozi waache maneno na kuweka tarehe za kazi kuanza kazi na si vinginevyo.
    Karne ya 21 si ya kufundisha na kushauri, ni karne ya vitendo.
    Mtoto Tanzania ni mtu mzima sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!