Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Ukraine yaondoa wanajeshi wake DRC
Kimataifa

Ukraine yaondoa wanajeshi wake DRC

Spread the love

UKRAINE imetangaza kuwaondoa vifaa vyake vya kijeshi pamoja na wanajeshi wake 250 katika Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa (UN) katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUSCO) ili kuilinda nchi yao dhidi ya uvamizi wa Urusi. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea)

Msemaji wa UN, Stephane Dujarric amethibitisha kupokea taarifa hiyo kutoka Ukraine kuhusu uamuzi wa kuwachukua wanajeshi wake.

Hata hivyo, tangazo la kujiondoa kwa kikosi cha Ukraine halionekani kuwatia wasiwasi raia wa mashariki mwa Kongo ambako wanajeshi hao wapo na ambako wakazi wanaathiriwa na ghasia za makundi yenye kumiliki silaha.

Kwa mujibu wa Idhaa ya Kiswahili Ujeruman (DW), ni kwamba kujiondoa kikosi cha Ukraine hakutakuwa na athari kwa amani katika eneo hilo kwani katika mkoa wa Ituri nchini Congo uliokumbwa na ghasia kwa miaka kadhaa, makundi yanayomiliki silaha yanawaua raia kila kukicha, licha ya kuwepo kikosi cha kulinda amani cha MONUSCO.

Mratibu wa mashirika ya kiraia mkoani Ituri, Dieudonné Lossa Dekhana amesema licha ya jeshi la MONUSCO kukaa katika mkoa huo wa Ituri kwa zaidi ya miaka 20, bado makundi yenye silaha yanaendelea kuongezeka.

“Usalama haupo kwa muda wote huo. Tunaamini kwamba iwapo jeshi la taifa FARDC litakuwa na vifaa muhimu, litafanya vizuri kuliko MONUSCO,” amesema.

Kauli hiyo imelandana na ya Katibu mkuu wa shirika la kiraia huko Beni nchini DRC John Kambale ambaye amesema kujiondoa kikosi cha Ukraine hakutaleta athari zozote, kwani kuwepo kwa vikosi vyote hivyo hakuna maana.

“Hawawezi kuendelea kubaki Kongo, watu wanaendelea kufa wakati MONUSCO wanaendelea kutazama. Kurudi kwao … sisi raia wa Beni, raia wa kawaida, tumeona wenzetu wakifa mbele ya macho yao, hatuwezi kushtuka wala kushangaa. “Tunawatakia safari njema. Sasa tunasubiri wenzao wanaobaki Kongo ndani ya MONUSCO nao waende kwenye nchi zao kwani hatuoni kazi zao,” amesema.

Aidha, naye Mbunge wa Kivu Kaskazini, Juvenal Munubo ambaye pia ni mjumbe wa tume ya ulinzi na usalama katika Bunge la Kitaifa, amesema ni jambo la kawaida Ukraine kuwaondoa wanajeshi wake ili kukabiliana na uvamizi wa Urusi.

Pia Juvenal Munubo ameiambia DW kwamba ni lazima Kongo ijitegemee.

“Tusiwategemee wageni, tusiitegemee MONUSCO kwani ni watu ambao walikuja kutusaidia. Kama tunakuwa na uregevu ndani ya sekta yetu ya usalama, hata msaada hautaleta manufaa.

“Ni lazima kwanza tulijenge jeshi letu, tuijenge polisi yetu, tuujenge ujasusi wetu na hapo tukipata msaada kutoka ugenini utakuwa na manufaa. Ni sharti tupambane na rushwa ndani ya jeshi, tuibadili sura ya jeshi letu, hapo tukipata msaada kutoka nchi rafiki italeta manufaa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!