Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wazawa kubebwa sasa basi, muswada kutua bungeni
Habari za SiasaTangulizi

Wazawa kubebwa sasa basi, muswada kutua bungeni

Spread the love

WAZIRI wa Kilimo, Hussein Bashe amesema hadi kufikia Juni mwaka huu amepanga kupeleka muswada wa sheria ili kuruhusu kampuni binafsi kutoka nje kuingiza sukari nchini kwa njia ya soko huria. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Amesema hatua ya Serikali kuwabeba wazawa katika  kuzalisha na kuingiza sukari nchini sasa imeonekana kutokuwa na faida hasa ikizingatiwa bidhaa hiyo ni sawa na usalama wa Taifa.

Akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo Alhamis Ikulu jijini Dar es Salaam amesema kampuni hizo za kitanzania, zimepewa msamaha wa kodi katika kuingiza  sukari lakini bado zimeshindwa kuziba pengo la uhaba wa sukari.

Waziri wa Kilimo Tanzania, Hussein Bashe

Aidha, Bashe amesema wizara hiyo imeupatia idhini Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA kuingia makubaliano na kampuni za nje kutoka nchi zinazozalisha sukari kwa wingi duniani kuingiza sukari nchini ili kumaliza tatizo la uhaba wa bidhaa hiyo kwa kuwa kampuni za uzalishaji sukari Tanzania zilizopewa kibali cha kuagiza bidhaa hizo, zimeshindwa kutekeleza jukumu hilo kwa ukamilifu.

Amesema hadi kufikia tarehe 10 Machi mwaka huu NFRA kwa kushirikiana na kampuni hizo itakuwa imeingiza tani 50,000 za sukari.

Akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habar leo Alhamisi Ikulu jijini Dar es Salaam, amesema mwaka huu tani 300,000 zitaingizwa.

Ametoa mfano kuwa viwanda cha TPC, Kagera na Kilombero vilipewa vibaki vya kuingiza tani 10,000 kila kimoja lakini hadi sasa kila kimoja kimeingiza tani zisizozidi 2000.

Amesena kiwanda cha Mtibwa sasa ndio sukari yake iliyoagizwa imeingizwa.

Amesema kiwanda pekee kilichoingiza sukari yote kwa mujibu wa kibali ni cha Bagamoyo kinachomilikiwa na mfanyabiashara maarufu, Saod Bahkera kwa kuingiza nchini tani zote 10,000.

“Viwanda vingine vimeingiza tani 300 tena jwa kuchangia kujaza meli. Kiujumla vibali tulivyowapatia wazawa hawa hakuna aliyezidi asilimia 20 ya malengo tuliyowapatia,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

error: Content is protected !!