Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa 84 mbaroni kuuza sukari bei ghali
Habari za Siasa

84 mbaroni kuuza sukari bei ghali

Spread the love

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe leo Alhamisi amesema jumla ya wafanyabiashara 84 wamekamatwa kutokana na kupandisha bei ya sukari. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari Ikulu jijini Dar es Salaam amesema wapo katika hatua ya mwisho kupeleka mahakamani wafanyabiashara hao.

Amesema licha ya wafanyabiashara kuuziwa sukari kwa bei ya Sh 2500 hadi 2800 kwa kilo bado wameenda kuuza 4500 hadi 5000.

“Machi 15, tutakuwa tumeingiza tani 60,000 za sukari hivyo wakati wa mfungo wa Ramadhani hali itakuwa imetengamaa,” amesema Bashe.

Aidha, amesema licha ya kwamba tayari tani 31,000 zimekwisha sambazwa nchini huku tani nyingine 25,000 zikiwa zimewasili katika katika bandari ya Dar es Salaam, kwa mwaka huu Serikali itaagiza tani 300,000 za sukari kukabiliana na uhaba wa sukari nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko aipongeza GGML kudhibiti vifo, majeruhi mahali pa kazi

Spread the loveNAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za Siasa

Askofu Shoo awataka ACT kupigania maslahi ya Taifa, wasikubali kuhongwa

Spread the loveALIYEKUWA Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Askofu...

Habari za Siasa

Biteko aagiza waajiri kudhibiti vifo mahali pa kazi

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

error: Content is protected !!