Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mramba: Mgawo wa umeme kuisha muda wowote
Habari za SiasaTangulizi

Mramba: Mgawo wa umeme kuisha muda wowote

Spread the love

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Felchesmi Mramba amesema tatizo kubwa la mgawo wa umeme unaondelea sasa halitokani na udhaifu katika miundombinu ya usambazaji wa umeme kama ilivyoelezwa jana Jumatano na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Amesema mwaka juzi Rais Samia Suluhu Hassan aliidhinisha Sh 1.9 trilioni kuimarisha mfumo wa usambazaji umeme kutoka kwenye gridi na Bunge limeidhinisha fedha hizo kila mwaka kuimarisha vifaa mbalimbali vya mfumo huo wa usambazaji na kujenga vituo vya kupoza umeme.

Hayo yamejiri baada ya Chalamila kuueleza umma kwamba tatizo la mgawo wa umeme linatokana na uchakavu wa miundombinu na kuongeza kwamba hata kama bwawa la Mwalimu Nyerere litaingiza umeme wake kwenye gridi ya taifa, tatizo la mgawo halitoisha.

Mhandisi Felchesmi Mramba.

Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari Ikulu jijini Dar es Salaam kuhusu hoja hiyo, Mramba ambaye alisita kumtaja moja kwa moja Chalamila, alisema hoja ya mkuu huyo wa mkoa kuhusu miundombinu ni kweli ipo ambayo ni chakavu ila haiwezi kusababisha mgawo wa umeme nchi nzima.

Amesema tatizo la mgawo wa umeme linatarajiwa kuisha muda wowote kuanzia sasa kutokana na kukamilika majaribio ya mashine ya kwanza ya kufua umeme wa Megawati 235 kutoka kwenye Bwawa la Mwalimu Nyerere.

Aidha, Mramba amesema tatizo kubwa la mgawo wa umeme unaondelea linatarajiwa kuisha muda wowote kuanzia sasa baada ya kukamilika kwa majaribio ya mashine ya kufua umeme wa Megawati 235 katika Bwawa la Mwalimu Nyerere.

Amesema megawati hizo zinatarajiwa kuingizwa muda wowote kwenye gridi ya Taifa na kupunguza mahitaji ya umeme kwa asilimia 80 kwa siku nchini.

Amesema ifikapo tarehe 15 Machi mwaka huu mashine ya pili itakuwa imekalimilika kufanyiwa majaribio hivyo kumaliza kabisa tatizo la mgawo wa umeme nchini.

Amesema changamoto za umeme zilizopo nchini ni katika uzalishaji na usambazaji hivyo tatizo la usambazaji ambalo litatokana na nguzo kuanguka au transfoma kuungua haliwezi kusababisha mgawo wa umeme bali litaathiri watu wachache wakati Tanesco ikifanyia marekebisho miundombinu husika.

1 Comment

  • Duh!
    Zile megawati 1,000 na zaidi zitatoka lini?
    Tuache kubabaishana.
    Ninaomba kila ukizungumzia Bwawa la Nyerere utuambie uwezo wake na ni nini kinachelewesha kufikia uwezo huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

error: Content is protected !!