Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wahariri wamkaanga bosi bodi ya sukari kwa ububu
Habari za SiasaTangulizi

Wahariri wamkaanga bosi bodi ya sukari kwa ububu

Spread the love

Mkurugenzi Mkuu, Bodi ya Sukari Tanzania Prof. Kenneth Bengesi ameonja joto la jiwe kutoka kwa wahariri mbalimbali wa vyombo vya habari baada ya kumchongea mbele ya Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kwamba hapokei simu wala kujibu ujumbe mfupi wa maneno ‘meseji’ kutoka kwa waandishi wa habari wanapohitaji kupata ufafanuzi kuhusu masuala ya bodi hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hayo yamejiri leo Alhamisi baada ya kuwasilisha taarifa ya hali ya sukari nchini ambapo pamoja na maswali aliyoulizwa, pia alihojiwa ni kwanini hapendi kutoa ushirikiano kwa vyombo vya habari vinapohitaji ufafanuzi kutoka kwake.

Akijibu swali hilo, Profesa Bengesi alianza kujitetea kuwa mara nyingi huwa ‘bize’ na vikao lakini akasisitiza kuwa hutoa ushirikiano kwa kualikwa kwenye stesheni mbalimbali vya runinga na redio jambo ambalo lilionekana kupingwa na wahariri wengi.

Huku ming’ono ikiibuka pamoja na vicheko kutoka baadhi ya wahariri na waziri Bashe, hali hiyo iliyoonekana kumtia joto, Profesa huyo aliendelea kujitetea kuwa si kweli kwamba hatoi ushirikiano kwa vyombo hivyo.

Hayo yanajiri wakati Taifa likikabiliwa na uhaba wa sukari ambao Bashe amesema unatarajia kuanza kuisha kuanzia Machi mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

error: Content is protected !!