Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Biashara Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas
BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the love

KAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation wameingia makubaliano kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10  nchini  ambao watakabidhiwa mitungi ya kupikia ya Oryx Gas ili kuwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Akizungumza wakati wakikabidhi mitungi ya gesi ya kupikia ya Oryx 50 kwa wauguzi katika hospitali ya rufaa ya Mwananyamala kati ya mitungi 1000 itakayotolewa na Kampuni hiyo, Mkurugenzi wa Kampuni ya gesi ya oryx Araman Benoite amesema makubaliano hayo yanalenga kuongeza matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa watanzania.

Amesema katika kampeni hiyo ya kuwezesha watanzania kuingia katika matumizi ya nishati safi ya kupikia, mpaka sasa tayari wameshatoa mitungi kwa wananchi zaidi ya 32,000 ili kusaidia lengo la kufikia asilimia 80 ya watumiaji wa nishati safi.

Amesema matumizi ya nishati safi ya kupikia inasaidia kuondoa hatari za kiafya kwa watumiaji wa kuni na mkaa kama nishati ya kupikia lakini pia hatari za kimazingira na ustawi wa jamii.

“Takribani watu 33,000 wanapoteza maisha nchini Tanzania kwa maradhi yanayotokana na kuvuta moshi unaotokana na mkaa au kuni hiyo ndio sababu ya Oryx gas kuja na suluhisho la kuwahamasisha wananchi kutumia gesi kwa matumizi ya kupikia”, amesema Benoite.

Ameeleza kuwa matumizi ya gesi yanaepusha wamama na watoto kuumika kubeba kuni hivyo kuepuka kujeuriwa na wanyama wakali wakiwa katika harakati za kutafuta kuni pia kuimarisha maisha ya wanawake na kuwalinda dhidi ya vitendo vya udhalilishaji.

“Kuanzia mwezi wa saba mwaka 2021 tumekuwa mstari wa mbele kuunga mkono utekelezaji wa mkakati wa serikali uliopewa nguvu na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan kwa lengo kwamba ifikapo mwaka 2033 asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia”, ameeleza.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel, Doris Mollel amesema katika makubaliano waliosaini na oryx watawafikia wauguzi 1000 ambapo watawapa mitungi na majiko ya gesi kama mabalozi kwa kina mama waweze kutumia nishati safi ya kupikia ikiwa ni programu ya miaka miwili.

Amesema mitungi hiyo itakwenda kwa wauguzi walioko maeneo magumu ambapo watakuwa wanawatembelea kwenye vituo vya afya na zahanati ili kuweza kuwafikia wafanyakazi ambao ni wauguzi wanaofanya kazi kubwa ya kuokoa maisha hususani ya mama na mtoto.

Awali Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala mkoani Dar es Salaam, Dk. Zavery Benela amesema hospitali hiyo  inakabiliwa na ongezeko la wagonjwa wa mifumo ya hewa. Kati ya wagonjwa wa nje 500 wanaofika kuonwa na madaktari bingwa asilimia 30 ya wagonjwa hao ni wa matatizo ya mfumo wa hali ya hewa.

Amesema matatizo hayo ya upumuaji kwa sehemu kubwa yanasababishwa na hali ya hewa pamoja na mazingira ya kuandaa chakula kutokna na kuni na mkaa.

Aidha, Dk. Benela amesema magonjwa ya mfumo wa hali wa hewa  yamekuwa changamoto hasa kwa watu wazima na watoto wa umri wa chini ya miaka mitano.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!