October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wauaji wa watoto Njombe wabainika

Spread the love

SERIKALI imesema tayari vyombo vya usalama vimeshawabaini watu wanaodaiwa kutekekeza mauaji ya kikatili ya watoto 10 katika Wilaya ya Njombe ambayo yametokana na imani za kishirikina. Anaripoti Danson Kaijage, kutoka Bungeni Dodoma … (endelea).

Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola aliyasema hayo jana, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mufindi Kusini (CCM), aliyetaka kupata kauli rasmi ya serikali kuhusu hatua ambazo zimechukuliwa na serikali baada ya kuibuka taharuki kutokana na mauaji hayo yanayoendelea.

“Tayari tumeshawabaini watu wanaotuhumiwa kutekeleza mauaji hayo kutokana na imani za kishirikina na Naibu Waziri wangu (Hamad Yusuph Masauni) yuko huko akiendelea kuchukua hatua. Mambo yatakuwa sawa na hatutacheza na watu wanaoichokoza serikali ya Rais John Magufuli, hawatakuwa salama,” alisema Waziri Lugola.

Waziri Lugola alisema tangu juzi Januari 28, 2019 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni yupo mkoani Njombe ambako anafanya vikao vya ndani na kamati za ulinzi ili kutafuta chanzo.

Kabla ya Lugola kuhoji kuhusu mauaji hayo, swali la msingi liliulizwa na Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mwantumu Dau Haji aliyetaja kujua serikali ina mpango gani wa kuwapatia askari Polisi stahili zao kutokana na baadhi ya askari kupandishwa vyeo lakini hawapati stahili zao kama inavyotakiwa.

Katika majibu yake, Waziri Lugola Jeshi la Polisi kama ilivyo Wizara na idara nyingine za serikali lilihusika na zoezi la uhakiki wa watumishi, zoezi ambalo lilisitisha marekebisho yoyote kwenye daftari la mishara, ajira mpya pamoja na upandishwaji vyeo kwa watumishi wa serikali.

“Baada ya zoezi hilo kukamilika tayari maofisa,wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali zaidi ya 8,440 waliokuwa na madai mbalimbali yakiwemo stahili za kupandishwa vyeo wamerekebishiwa mishahara na stahili zao.

“Pia maofisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali wapatao 2,143 kati ya 3,089 walipandishwa vyeo mwezi Juni, Septemba na Desemba 2018 wamerekebushiwa mishahara yao, hata hivyo taratibu za kukamilisha kuwarekebishia askari waliobakia zinaendelea.”

error: Content is protected !!