March 5, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Sugu amshauri Rais Magufuli kumhamisha RC wa Mbeya

Dk. Mpoki Ulisubisya, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya

Spread the love

MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amesema kama angepata nafasi ya kumshauri Rais John Magufuli, angemshauri kumteua aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dk. Mpoki Ulisubisya kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya badala ya kumteua kuwa balozi. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Akizungumza Bungeni jijini Dodoma leo tarehe 30 Januari 2019 Sugu amesema Dk. Mpoki ni mchapakazi hivyo kitendo cha Rais Magufuli kumteua kuwa balozi, ni sawa na kuipeleka mbali huduma muhimu kwa taifa.

 “Kama ningeweza kumshauri rais, ningemshauri Dk. Mpoki kuliko kuwa balozi aletwe kuwa mkuu mkoa wa Mbeya kuliko kumpeleka mbali, kumpeleka mbali ni kupelekea mbali huduma kwa taifa,” amesema Sugu.

Katika hatua nyingine, Sugu ameipongeza wizara ya afya kwa kufanikisha ujenzi wa jengo la X-Ray katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya.

Aidha, ameiomba wizara ya afya kuondoa changamoto ya uhaba wa wataalamu wa afya hasa madaktari bingwa.

error: Content is protected !!