Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Watumishi wahimizwa kutumia TEHAMA
Habari Mchanganyiko

Watumishi wahimizwa kutumia TEHAMA

Spread the love

WATUMISHI wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) wamehimizwa kufanya kazi kwa kutumia TEHAMA, ili kufanikisha malengo ya serikali ya kutoa huduma bora na kwa haraka kwa jamii.

Kauli hiyo imetolewa jana tarehe 9 Julai, 2022 na Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Mussa Mbura wakati akifunga Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa Kituo cha Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mussa Mbura (wapili kulia) akisoma bango la namba ya mawasiliano ya bure kwa wadau wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), kabla ya kuizindua rasmi ikiwa ni kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma

Amesema TEHAMA inafaida kubwa na inarahisisha mambo mengi, ambayo yanaweza kufanyika kwa haraka na kwa kutumia muda mfupi.

Hata hivyo, amesema TEHAMA iende mbali Zaidi ya kutumia kwa shughuli binafsi, pia itumike katika utendaji wa watumishi ikiwa ni katika kuripoti masuala mbalimbali na pia  ukusanyaji wa mapato, ambayo anauhakika yataongezeka mara dufu.

“Imenisikitisha sana kusikia kuwa kuna mtu hana email address (anwani ya baruapepe), TEHAMA inarahisha mambo mengi na faida zake ni nyingi hivyo hata Wiki hii ya Utumishi inapomalizika tuendelee kuwahamasisha watumishi wetu wawe na anwani hizi

Hata hivyo, amesema Wiki hii ya Utumishi wa Umma yenye kaulimbiu ya mwaka huu ni “Nafasi ya Mapinduzi ya Nne ya Viwanda katika masuala mapya yaliyojitokeza kuhusu utoaji wa Huduma na urejeshwaji wakati baada ya Janga la Corona”, .imelenga kukusanya maoni, ushauri na malalamiko kutoka kwa wadau wa ndani na nje ya mamlaka, ambapo baadae kufanyiwa kazi kwa lengo ya kuboresha huduma kwa wadau hao.

“Hii kaulimbiu inatulenga sisi pia kama JNIA tuweze kuona baada ya janga la Corona tunafanyanini na kazi zetu tunazifanyaje na je utumishi wetu unakuwaje na tuangalie Zaidi katika kaulimbiu hii kwa kuangalia masuala ya viwanda na huduma tunazotoa kwa wananchi tukiwa kama watumishi wa umma baada ya Covid19 tuone tunaendaje mbele,” amesema Mkurugenzi Mbura.

Pia amesema anaimani wananchi waliopita kwenye banda la maonesho la JNIA wameweza kupata maelezo mbalimbali zikiwemo huduma zinazotolewa hapa, kwa kuwa wengi wanajua kwenye kiwanja hichi watu husafiri pekee, ambapo pia amewapongeza watumishi kwa kiwanja hicho kwa kufanyakazi kwa bidi na abiria wameendelea kusafiri.

Halikadhalika, ameipongeza JNIA kwa kufanya vyema kwenye Wiki hiyo ya Utumishi kwa kuwatembelea watumishi mahala pa kazi na kuhamasisha mfumo mpya wa serikali unaotambulika kama e-Mrejesho ambao unatumiwa na wananchi wote kuwasilisha masuala mbalimbali serikalini kwa ajili ya kupatiwa mrejesho.kwa haraka.

“Kimisingi nawapongeza JNIA kwa kufanya kazi kwa bidii ambapo abiria nikiwa na maana ya watalii na wawekezaji wameweza kuwasili kupitia hapa, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan baada ya kufanya filamu ya Royal Tour kwa kweli namba ya watu wanaopita kwenye airport zetu ni kubwa sana hivyo tumshukuru Mhe. Rais kwani ile adhima na ndoto yake sisi tuifanye kwa vitendo, kwani bado tunategemea wageni wengi Zaidi kwa miezi hii ijayo hivyo tuendelee kufanya kazi kwa bidii na kuongeza ari na tutumie mifumo ya TEHEMA ili tuwe tunakwenda haraka katika kutoa huduma,” amesema Mkurugenzi Mbura.

Pia awataka watumishi wa JNIA kuhakikisha wanakuwa wakarimu kwa wateja na kuwahudumia watu vizuri, ili wakati mwingine waweze kurudi kutumia kiwanja hiki na vingine vilivyopo nchini.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa JNIA, Mhandisi Rehema Myeye, awali akimkaribisha Mkuruigenzi Mkuu amesema maadhimisho hayo yamekuwa na mafanikio makuibwa, ambapo watumishi pamoja na wadau wanaotumia na kufanya shughuli mbalimbali kwenye kiwanja hicho walipata maelezo na ufafanuzi mbalimbali kutoka kwa maafisa wa vitengo mbalimbali waliokuwa kwenye banda la maonesho lililokuwa mbele ya Jengo la Pili la Abiria TB2).

Mhandisi Myeya pia amesema watumishi wamekumbushwa haki zao na pia wajibu wao kwa TAA katika utendaji wa kazi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

error: Content is protected !!