Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko PURA wamwaga ajira kwa kila kada ya elimu, wasiosoma
Habari Mchanganyiko

PURA wamwaga ajira kwa kila kada ya elimu, wasiosoma

Omary Mrisho (katikati) akizungumzia fursa za PURA
Spread the love

 

WANAFUNZI na wadau mbalimbali wametakiwa kuchangamkia fursa ya ajira katika Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) kwani taasisi hiyo ina uwanja mkubwa wa kutoa ajira kwa kada tofauti tofauti. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Wito huo umetolewa jana na Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kitivo cha Sayansi ya Kilimo na Teknolojia ya vyakula ambao wanasoma kozi Uchumi wa kilimo, Maliasili na Biashara walipotembelea banda la PURA lililopo katika maonesho ya Biashara ya kimataifa ya 46 yanayoendelea Katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Katibu wa Chama cha Dar es Salaam University Agribusiness and Natural Resources Economic Association, Omary Mrisho amesema moja ya mambo ambayo wameyagundua katika ziara ya kutembelea banda la PURA ni mamlaka hiyo kutoa ajira kwa wingi wanafunzi wenye elimu ya ngazi tofauti tofauti na hata wale ambao hawana elimu.

Omary amesema PURA inaajiri watu mbalimbali wenye elimu mpaka za juu lakini pia wanachukua hata mtu yule ambaye hajasoma kabisa kwa sababu kuna mgawanyiko wa kazi kulingana na mtu alichosomea.

“Kufanya kazi PURA siyo lazima mpaka uwe umesomea, injinia, kuna vitengo vingi ambayo masomo yake ni ya tofauti na injinia. Fursa ipo kubwa sana. Wapo wanaoajiriwa kwa ujuzi wao kulingana na mahataji, lakini hata asiyekuwa na elimu pia kuna kazi ambazo anaweza kufanya katika mamlaka hii,” amesema Omary.

Katibu huyo amesema mbali na kugundua fursa za ajira zilizopo ndani ya PURA pia wamejifunza uhalisi wa kile ambacho wamekuwa wakikisoma darasani katika maisha ya kawaida.

Pia aliwashauri wanafunzi wengine kuwa na moyo wa kutaka kujifunza kitu badala ya kukaa darasani na kusubiri pekee watoke nje ili wapate fursa ya kujifunza zaidi kwa vitendo na uhalisia wenyewe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

error: Content is protected !!