Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Rais Samia amlilia Bi Hindu
Habari Mchanganyiko

Rais Samia amlilia Bi Hindu

Chuma Selemani maarufu kama ‘Bi Hindu’
Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema amepokea kwa huzuni taarifa ya kifo cha muigizaji mkongwe Chuma Selemani (Bi Hindu). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (emdelea).

Rais ameyasema hayo leo tarehe 9 Julai, 2022 kupitia taarifa fupi aliyoitoa katika mtandao wa Twitter huku akitoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki kwa msiba huo.

“Nimepokea kwa huzuni kubwa taarifa za kifo cha msanii maarufu wa Kaole, Chuma Selemani maarufu ‘Bi Hindu’.

“Uweledi wake wa uigizaji na matumizi ya lugha ya Kiswahili yalileta mvuto kwa watazamaji wa Rika zote. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema Peponi. Amin,” amesema Rais Samia.

https://youtu.be/Y060_sjaxWM

Kwa mujibu wa taarifa iliyothibitishwa awali na mwanaye alisema kuwa, mama yake alifariki akiwa nyumbani kwake Magomeni katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Alisema, Bi Hindu alikuwa akisumbuliwa na saratani ya mapafu kwa muda mrefu hadi umauti ulipomkuta. Mwenyenzi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

AfyaHabari Mchanganyiko

200 wapimwa afya na GGML katika maonesho ya OSHA

Spread the loveZAIDI ya watu 200 jijini Arusha wamejitokeza kupimwa afya na...

error: Content is protected !!