Saturday , 4 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Watumishi wa ardhi watakiwa kutatua migogoro ya ardhi
Habari Mchanganyiko

Watumishi wa ardhi watakiwa kutatua migogoro ya ardhi

Spread the love

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Geophrey Pinda amekutana na kuzungumza na watumishi wa Wizara hiyo pamoja na watumishi wa Idara ya Ardhi kutoka jiji la Dodoma ambapo amewataka kuwahudumia wananchi kutatua migogoro ya ardhi katika maeneo yao. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Naibu Waziri Pinda amesema hayo jana Jumatano jijini Dodoma katika kikao cha kuhitimisha huduma za Kliniki ya Ardhi kilichofanyika katika Ofisi za Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Dodoma kuanzia tarehe 4 Novemba  hadi 12 Desemba  2023.

“Onesheni utaalamu wenu, fanyeni kazi kwa vitendo ya kuwahudumia wananchi, badilikeni, fanyeni kazi kwa weledi na tambulikeni kwenye jamii kwa kuwa mfano bora kwa utendaji kazi wenu” amesema Pinda.

Aidha, Pinda amewataka Wapima Ardhi, Wathamini, Maafisa Mipango Miji pamoja na Maafisa Ardhi kuendelea na moyo wao wa uzalendo waliouonesha wakati wote wa Kliniki hiyo na kuwahimiza kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, taratibu na miongozo ya utumishi wa umma katika maeneo yao ya kazi hata uwandani wanapoenda kuwahudumia wananchi katika maeneo mbalimbali katika jiji la Dodoma.

Awali akimkaribisha Naibu Waziri, Katibu Mkuu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Antony Sanga amepongeza watumishi hao kwa kufanyakazi ya kutoa huduma kwa Watanzania katika Mkoa wa Dodoma.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, John Kayombo amesisitiza watumishi wa Idara ya Ardhi katika jiji hilo kufanya kazi kulingana na taaluma zao bila kuingilia taaluma ya mtu mwingine kwa kufanyakazi kwa ushirikiano na kuwahimiza wakawe wapya katika kutoa huduma kwa wananchi baada ya kumaliza kliniki hiyo.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Geophrey Pinda

“Watumishi wenzangu, tufanye kazi kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan, hatuhitaji kutengeneza migogoro, tunahitaji kutatua migogoro ya ardhi yote iishe, kazi zinatupa heshima” amesema Kayombo.Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya watumishi hao, Kamishna Ardhi nchini, Nathaniel Mathew Nhonge amesema wamepokea maelekezo ya viongozi na watayatekeleza ili kufanikisha malengo ya Serikali ya kuwahudumia wananchi.

1 Comment

  • Hati halali zipo wizarani, kwa nini hamuandiki barua rasmi kumjulisha asiye na ardhi. Kwa kutokufanya hivyo mafisadi wamekuwa wanapeleka kesi mahakamani nyinyi mamuendi.
    Mtakiwe kuwepo mahakamani kila kesi inapotajwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari MchanganyikoTangulizi

Usafiri baharini wasitishwa kukwepa athari za kimbunga Hidaya

Spread the loveUSAFIRI wa baharini umesimamishwa kwa muda ili kukwepa athari za...

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

error: Content is protected !!