Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wateule wa Rais wapendekezwa kuteua wajumbe Tume ya Taifa ya Uchaguzi
Habari za Siasa

Wateule wa Rais wapendekezwa kuteua wajumbe Tume ya Taifa ya Uchaguzi

Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma
Spread the love

KIKOSI Kazi cha kukusanya maoni ya wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini Tanzania, wamependekeza kuwepo kwa kamati maalumu itakayoteua wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Waliopendekezwa kuunda kamati hiyo ni Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania ambaye atakuwa Mwenyekiti, Jaji Mkuu wa Zanzibar ambaye atakuwa Makamu Mwenyekiti, Kamishna wa Sekretarieti ya Madili ya Viongozi wa Umma wa Tanzania bara, Mwenyekiti wa Tume ya Maaadili ya viongozi wa umma ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu. Wote hawa ni wateule wa Rais.

Kikosi kazi pia kimependekeza kuwa wajumbe wengine wawili wateuliwe na Jaji Mkuu wa Tanzania kutoka kwa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na Chama cha Wanasheria Zanzibar.

Wadau wa siasa nchini vikiwemo vyama vya siasa, wamekuwa wakilalamikia utaratibu wa sasa wa uteuzi wa wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuteuliwa na Rais ambaye pia huwa ni mgombea wakati wa Uchaguzi Mkuu na hivyo kuleta mgongano wa kimaslahi.

Wanaoteuliwa na Rais katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni pamoja na Mwenyekiti, Mkurugenzi na Makamishna wa Tume.

Aidha Wakurugenzi wa Halmashauri ambao pia ni wateule wa Rais ndiyo wasimamizi wa Uchaguzi katika ngazi za Halmashauri ambapo wengi wao wanadaiwa kuwa wanachama na makada wa Chama Cha Mapinduzi.

Mbali na uteuzi wa wajumbe wa Tume, kikosi kazi hicho ambacho kimewasilisha ripoti yake leo Ijumaa, pia kimependekeza uamuzi wa Tume kuhojiwa katika Mahakama ya Juu pale itakapoundwa pamoja na maofisa wao kuwajibishwa pale watakapokiuka Sheria na Taratibu za Uchaguzi.

Pia kimependekeza kuongezwa kwa matumizi ya TEHAMA katika uchaguzi ikiwemo vifaa na wataalamu watakaosaidia uchaguzi ufanyike kwa njia hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!