Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Majaliwa atoa siku 15 mkandarasi kukamilisha barabara Ukerewe
Habari za Siasa

Majaliwa atoa siku 15 mkandarasi kukamilisha barabara Ukerewe

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa
Spread the love

 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa siku 15 kuanzia Oktoba 20, 2022 kwa kampuni ya Inter Country Contractors kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa miradi ya barabara katika kisiwa cha Ukerewe mkoani Mwanza. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza … (endelea)

Majaliwa ametoa agizo hilo jana Alhamis tarehe 20, Oktoba, 2022, alipokutana na Waziri wa Nchi -OR TAMISEMI, Viongozi wa Wilaya ya Ukerewe na Watendaji wa TARURA ofisini kwake Mlimwa jijini Dodoma.

Waziri Mkuu amesema kuwa kampuni hiyo ilipewa kandarasi ya ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilomita 13 kwa kiwango cha lami na changarawe katika kisiwa hicho ambapo ilipaswa kukamilisha kazi hiyo Julai 2022.

“Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan inatoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara, katika hili tumetoa kipaumbele kwa wakandarasi wazawa, tunachotegemea ni uaminifu wenu na utekelezaji wa miradi hii iwe ya viwango na mkamilishe kwa wakati”

 Majaliwa amesema ni vyema Mameneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) Mikoa na Wilaya wakatekeleza majukumu yao ipasavyo ili kuhakikisha ujenzi wa barabara katika maeneo mbalimbali nchini na ukamilika kwa wakati na kwa viwango vilivyokusudiwa.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Angellah Kairuki amesema wamepokea maelekezo ya Mheshimiwa Waziri Mkuu na kuahidi kufanya mapitio makubwa ya mfumo wa kiutendaji wa TARURA ili kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa miradi ndani ya taasisi hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

error: Content is protected !!