Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Biashara Wateja 100 wazoa mil. 10 ‘NMB MastaBata Halipoi’
Biashara

Wateja 100 wazoa mil. 10 ‘NMB MastaBata Halipoi’

Spread the love

KAMPENI ya Weka, Tumia ana Ushinde inayoendeshwa na benki ya NMB ikilenga kuhamasisha matumizi yasiyo ya pesa taslimu, imezidi kuchanja mbuga, baada ya jana Alhamisi kuchezeshwa kwa droo ya tisa, iliyozalisha washindi 100 waliojinyakulia Sh10 milioni (sawa na Sh 100,000 kila mmoja). Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea)

Idadi ya washindi 100 wa droo hiyo, inafanya wateja wa benki hiyo waliojinyakulia zawadi za wiki kufikia 900 kati ya 1,200 waotarajia kujishindia kiasi cha Sh 100,000 kila mmoja katika kipindi cha miezi mitatu ya kampeni hiyo ijulikanayo kama ‘NMB MastaBata Halipoi,’ iliyozinduliwa tarehe 27 Oktoba mwaka 2023.

Meneja wa Benki ya NMB Kitengo cha Kadi, Sophia Mwamwitwa (mwenye kipasa sauti) akimwonesha mmoja wa wateja wa NMB Tawi la Magomeni, Eva Kapembe ushahidi wa muamala wa kumuingizia kiasi cha Sh 50,000 mara baada ya kujishindia kiasi hicho cha fedha katika bahati nasibu ya papo hapo iliyochezeshwa sambamba na washindi wa droo ya wiki ya tisa ya Kampeni ya Kuhamasisha Matumizi yasiyo ya pesa taslim ‘NMB MastaBata Halipoi’. ambapo washindi 100 walijishindia shilingi milioni 10. Kushoto ni Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Rasuli Masoud, na Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Magomeni, Mary Marungi (katikati) wakifuatilia.

Ukiondoa washindi 1,200 wa kila wiki, NMB MastaBata Halipoi – kampeni yenye zawadi mbalimbali zenye thamani ya Sh. mil. 350, inatoa pia washindi 30 wa mwisho wa mwezi (washindi 15 kwa kila mwezi wanaojizolea Sh500,000 kila mmoja), washindi 240 wa Papo kwa Papo wanaopata Sh50,000 kila mmoja.

Akizungumza wakati wa droo hiyo iliyoendeshwa chini ya usimamizi na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Rasuli Masudi, Meneja wa NMB Tawi la Magomeni ilikochezeshwa droo hiyo, Mary Marungi alisema wateja wa Papo kwa Papo wanaozawadiwa ni wale watakaokutwa wakifanya manunuzi kwa kadi.

“Pia tunawazawadia washindi 10 na wenza wao ambao wapata fursa ya Kwenda kuhudhuria Tamasha la NMB Full Moon Party linalofanyika Kendwa Rocks Hotel, Zanzibar, safari iliyogjharamiwa kila kitu na NMB, pamoja na kupewa pesa ya matumizi binafsi ya Sh 200,000 kila mmoja.

“Kampeni hii itahitimishwa kwa washindi 12 na wenza wao kufanya safari ya utalii mjini Cape Town nchini Afrika Kusini, gharama zote zikiwa zimelipiwa na NMB, ambako watakula bata kwa siku tano,” alisema Marungi wakati wa ufunguzi wa droo hiyo iliyoambatana na zawadi kwa wateja waliokuwa wakihudumiwa tawini hapo.

Aidha, Marungi alibainisha kuwa nia ya NMB MastaBata Halipoi ni kuifanya jamii kuendana na kasi ya teknolojia, wanakowapa msisitizo wa kufanya manunuzi na malipo kwa kutumia NMB MasterCard, Lipa Mkononi (QR Code) na Vituo vya Mauzo (PoS) na malipo ya mtandaoni na yale ya kwenye vituo vya mafuta, ‘supermarket’ na migahawa mbalimbali.

Kwa upande wake, Masudi kutoka GBT aliipongeza NMB kwa kudumisha utamaduni chanya wa kuzawadia wateja wao waliouanza mwaka 2018 ilipozindua kampeni hiyo na kwamba wateja wa benki hiyo wanapaswa kushiriki matumizi ya kadi ili kujihakikishia nafasi za kushinda peza taslimu na safari za kitalii ndani nan je ya nchi.

“Sisi GBT tunawapongeza NMB kwa hiki inachofanya kwa msimu wa tano sasa, inaonesha namna inavyowajali wateja wao kwa kuwazawadia kila wanapoweka akiba na wanapofanya matumizi. Jukumu letu ni kusimamia na tunawahakikishia wote kwamba droo hizi zinafanyika kwa kufuata vigezo na masharti, hakuna ujanja ujanja,” alibainisha Masudi.

Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Magomeni, Mary Marungi (wa pili kulia) akimkabidhi mmoja wa washindi wa papo hapo zawadi ya kofia ya NMB aliyojishindia mara baada ya kukamilisha droo ya wiki ya tisa ya Kampeni ya Kuhamasisha Matumizi yasiyo ya pesa taslim ‘NMB MastaBata Halipoi’ ambapo washindi 100 walijishindia Sh milioni 10. Kushoto ni Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Rasuli Masoud pamoja na Meneja Huduma za Kadi, Ednamamu Mshubi wakifuatilia.

Droo hiyo ya 9 iliyoshuhudiwa pia na Meneja wa Kitengo cha Kadi NMB, Sophia Mwamwitwa na Meneja Huduma za Kadi NMB, Ednamamu Mshubi imefanyika wiki moja tu tangu wateja 15 walipojinyakulia zawadi ya Sh. 500,000 kila mmoja katika droo ya piliya mwisho wa mwezi iliyofanyika Desemba 29 jijini Arusha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yashiriki maadhimisho Mei Mosi Arusha

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na maelfu ya...

Biashara

Promosheni ya bil 1 kutoka Meridianbet kasino, cheza na ushinde zawadi kubwa

Spread the love  INGIA katika ulimwengu wa zawadi za kushangaza: Jishindie sehemu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Equity Bank yaendelea kusotea mabilioni ya fedha mahakama rufani

Spread the loveBENKI za Equity ya Tanzania na Kenya, zimeendelea kupambana mahakamani...

error: Content is protected !!