Saturday , 30 September 2023
Home Kitengo Michezo Wanne kuiwakilisha Tanzania chaguo la awali Future Face
Michezo

Wanne kuiwakilisha Tanzania chaguo la awali Future Face

Spread the love

 

WANAMITINDO wanne kati ya 200 waliojitokeza kwenye usaili wa Shindano la Future Face 2023 wameteuliwa kuiwakilisha Tanzania kwenye chaguo la awali la Future Face duniani 2023. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Usaili wa shindano hilo la Future Face umefanyika kwa kushirikiana na kuratibiwa na Mwanamitindo wa kimataifa, Millen Happiness Magese jijini Dar es Salaam huku majaji wa nne wakihusika katika kuchuja wanamitindo waliojitokeza hadi kubakia na wawakilishi wanne kati ya hao 200 waliojitokeza.

Majaji katika usaili wa shindano hilo la kimataifa ambalo ndio mara ya kwanza kufanyika nchini Tanzania walikuwa Ally Rehmtullah, Mwanamitindo wa Kimataifa Millen Happiness Magese, Martin Kadinda na Jamilla Vera Swai.

Akitangaza matokeo ya usaili huo Mwanamitindo Magese amesema kuwa vijana zaidi ya 200 walijitokeza kwenye usaili uliofanyika mwishoni mwa wiki.

Amesema baada ya kuangalia sifa na vigezo vya Shindano hilo wamefanikiwa kuwapata wawakilishi wa nne ambao hao watachuana tena na kumpata mmoja ambaye ataiwakilisha nchi ya Tanzania katika mashindano hayo.

Amewataja walioteuliwa kwenye usahili huo ni Rachel Amani Julius(20) – 5’8 Ft, Joyceller Lasway(25l – 5’9 Ft, Neema Evaresty(23) – 5’11 Ft pamoja na Jasinta David Makwabe(25) – 5’11 Ft.

Magese amesema baada ya kupatikana kwa wawakilishi hao hakutakuwa na kambi huku akifafanua yule atakayechaguliwa kuiwakilisha nchi Septemba mwaka huu atakwenda nchini na Nigeria na akifanikiwa kushinda anakwenda nchini Ufaransa au Italia.

“Nawashukuru majaji wote kwa ushiriki na kujitoa kwao kufanikisha jambo hili muhimu ambalo limeandika historia kubwa katika nchi yetu kwani ndio mara ya kwanza Shindano la Future Face linafanyika nchini Tanzania.

” Pia nawashukuru sana vijana wote kwa kujitokeza kwa wingi, sikutegemea kuona umati uliojitokeza na kama mtu hakuweza kufika basi anaruhusiwa kutuma maomba yake kwa njia ya mtandao kupitia www.futurefaceglobal.com ambapo mwisho ni tarehe 22 Septemba 2023″ amesema.

Awali wakati anazungumzia Shindano hilo, Mwanamitindo huyo amesema ameshirikiana na Future Face kuleta Shindano hilo kubwa zaidi la kimataifa la kusaka wanamitindo mwaka wa 2023.

Amesema Shindano hilo ni la kipekee lililoandaliwa na Wakala mkubwa zaidi wa wanamitindo barani Afrika, Beth Model Management na limekuwa na utofauti wake wa ukubwa, umri, rangi na kabila, na ulemavu, huku shindano likiwa na sera ya fursa sawa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Meridianbet yaibukia Tandika, yafungua duka jipya

Spread the love BAADA ya kupita maeneo mbalimbali hatimae kampuni yaMeridianbet imeibukia...

BiasharaMichezo

Ukiwa na Meridianbet ni rahisi kuwa milionea

Spread the love  CARABAO Cup raundi ya 3 Uingereza inaendelea na mechi...

Michezo

Jezi ya Samatta iliyoifunga Liverpool kuuzwa Genk

Spread the love  KLABU ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji imeamua kuanza...

BiasharaMichezo

Hii ndio historia ya El-Clasico, derby bora zaidi duniani

Spread the love  KILA nchi ina vilabu viwili hasimu na pinzani nje...

error: Content is protected !!