MWENYEKITI wa Chama Cha Demokrasia na Maendelo- CHADEMA, Freeman Mbowe, amesema kuwa zaidi ya asilimia 60 ya maeneo ya ukanda wa Ziwa Victoria, hayana maji safi na salama. Anaripoti Isaya Temu, TURDARco … (endelea).
Jana tarehe 9 Agosti 2023 , Kupitia ukurasa wake rasmi katika mtandao wa kijamii wa X zamani Tweeter, Mbowe amesema maeneo yote waliyozunguka Chama cha Demokrasia na Maendeleo wamekuta yana shida ya maji safi na salama pamoja na kuwa karibu na Ziwa Victoria.
“Maeneo yote ya ukanda wa Ziwa Victoria tuliyopita, zaidi ya asilimia 60 hayana maji safi na salama. Ziwa Victoria linawanufaisha watu wa Misri na nchi nyingine. Geita mjini, Geita vijijini, Nyarugusu, kote huko wana utajiri mkubwa wa dhahabu lakini hawana maji. Wanakunywa maji yasiyo salama yanayochanganyika na madini yenye sumu ya zebaki inayotumika kwenye shughuli za madini,” ameandika Mbowe.
Maeneo yote ya ukanda wa Ziwa Victoria tuliyopita, zaidi ya asilimia 60 hayana maji safi na salama. Ziwa Victoria linawanufaisha watu wa Misri na nchi nyingine. Geita mjini, Geita vijijini, Nyarugusu, kote huko wana utajiri mkubwa wa dhahabu lakini hawana maji. Wanakunywa maji… pic.twitter.com/SfBrlHvVuN
— Freeman Mbowe (@freemanmbowetz) August 8, 2023
Pia Mwenyekiti huyo cha CHADEMA alieleza shida kubwa inayosababisha ukosefu wa huduma hiyo ya maji Kanda ya Ziwa ni kutokana kuwa na Viongozi wa CCM ambao wameshidwa kuwa na mipango thabiti na kugeuza rasilimali kuwa laana.
“Uongozi mbovu wa CCM umegeuza utajiri mkubwa wa raslimali kuwa a curse of resources (laana ya rasilimali), ameongeza Mbowe
CHADEMA bado kipo maeneo ya kanda ya ziwa kwa ajili ya kufanya mikutano ya hadhara na wananchi kwa ajili ya kutoa elimu kuhusiana na mambo mbalimbali ikiwemo sakata la mkataba wa bandari.
Leave a comment