Wednesday , 8 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wananchi walianzisha, polisi waanza msako
Habari Mchanganyiko

Wananchi walianzisha, polisi waanza msako

Spread the love

WAKAZI wa Mtaa wa Nyakabungo “A” katika Kata ya Isamilo, Nyamgana jijini Mwanza, ‘wamemuhukumu’ Selina Francis (50) na Abdallah Mwita kwa kuchoma moto nyumba zao. Anaandika Mwandishi Wetu, Mwanza …(endelea).

Tukio hilo lilitokea jana usiku saa 3 (Julai 25, 2018) ambapo nyumba inayomilikiwa na Selina maarufu kwa jina la Mama Mkapa na ile ya Abdallah anayetambulika zaidi kwa jina la Machela zilichomwa moto na wananchi hao.

Mtoto wa Selina aitwaye Mkapa Mwabe na yule wa Abdallah anayetajwa kwa jina la Emmanuel wanatuhumiwa kujihusisha na uhalifu na pale wanapopelekwa kwenye vyombo vya sharia, huachwa na kurejea mtaani kuendelea na matukio hayo.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya wananchi ‘kuchoshwa’ na watoto wa wenye nyumba hao kuendelea kuwepo mitaani licha ya juhudi kufanyika za kuwahamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria kutokana kujihusisha na matukio ya uhalifu mara kwa mara kufeli.

“…ni kwa kuwa, vijana hawa wamekuwa wakipelekwa polisi na hata mahakamani lakini hurudi mtaana na kuendelea na vitendo vya kihalifu. Watu wakaona bora wawatie adabu wazazi wao,” amezungumza Zubeir Mwevi, mkazi wa Mwanza.

Hata hivyo, dhahama hiyo pia ilielekezwa kwenye nyumba ya Manka Francis James kwa jina maarufu Mushi ambapo iliharibiwa vibaya kwa kuvunjwa madirisha na milango pamoja na vitu mbalimbali kwa madai ya mama huyo kuhusika kuwaficha wezi.

Tuhuma zingine zilizodaiwa na wananchi hao ni mama huyo kujihusisha na utapeli wa kuwauzia watu dhahabu bandia.

Watu hao walifika kwenye nyumba ya Manka na kuwatoa watoto ndani kisha kuwaweka mahali salama na kuanza kushambulia nyumba hiyo.

Jeshi la Polisi baada ya kupata taarifa hiyo liliwasili eneo la tukio ambapo sasa linaendesha msako kuwatafuta waliohusika na matukio ya uchomaji nyumba pamoja na wale wanaotuhumiwa kufanya uhalifu.

Ahmed Msangi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza ameonya watu wanaojichukulia sharia mkononi na kwamba, watakutana na mkono wa sharia.

“Dmana ni haki ya mtuhumiwa,” amesema Kamanda Msangi na kwamba, dhamana hupewa mtuhumiwa pale tu kesi anayohumiwa nayo inadhaminika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

error: Content is protected !!