Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Wanafunzi 3,000 MNMA wafundwa uongozi, maadili
Elimu

Wanafunzi 3,000 MNMA wafundwa uongozi, maadili

Spread the love

CHUO cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA), kilichopo wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam, kimetoa mafunzo ya uongozi na maadili kwa wanafunzi wanaotarajia kumaliza masomo ya ngazi mbalimbali chuoni  hapo mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Mafunzo hayo yametolewa kwa siku tano chuoni hapo kuanzia Julai 10 hadi 15 mwaka huu ambapo zaidi ya wanafunzi 3,000 wanaotarajiwa kuhitimu shahada ya kwanza, diploma na cheti wamenufaika.


Akifungua mafunzo hayo ya siku tano, Naibu Mkuu wa Chuo anaesimamia Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Profesa Richard Kangalawe amesema lengo la mafunzo hayo ya uongozi na maadili ni kuwajengea uwezo wanafunzi waweze kujitambua na kujua uhuru wao, haki na wajibu na  kuwa wazalendo katika nchi yao.

Naibu Mkuu huyo wa Chuo amesema chuo kwa sasa kimeanzisha Mitaala ya Kozi za muda mrefu kuanzia ngazi ya Cheti mpaka Shahada ya Pili katika Mafunzo ya Uongozi na Maadili.

“Mafunzo hayo yanatolewa kwa Wanafunzi zaidi ya 3,000 wanaotarajiwa kuhitimu kozi mbalimbali za Shahada ya Kwanza, Diploma na kozi ya Cheti kwa mwaka wa masomo 2022/23.

Baada ya mafunzo hayo wahitimu watatunukiwa vyeti vya uongozi  na maadili,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari Mchanganyiko

Chongolo aagiza TAKUKURU kuchunguza ujenzi wa bweni

Spread the loveMkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amemuagiza Kamanda wa...

ElimuHabari Mchanganyiko

Ugawaji taulo za kike watajwa kutokomeza utoro shuleni

Spread the loveBAADHI ya wanafunzi na walimu wa shule za sekondari mkoani...

ElimuHabari za Siasa

MbungeCCM ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the love  MBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze...

ElimuHabari za Siasa

Walimu 52,551 kupandishwa madaraja mwaka huu

Spread the loveNaibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala...

error: Content is protected !!