Saturday , 22 June 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Walinzi mpaka wa Saudi Aradia watuhumiwa kuua wahamiaji
Kimataifa

Walinzi mpaka wa Saudi Aradia watuhumiwa kuua wahamiaji

Spread the love

Shirika la Kutetea Haki za Binadamu (Human Rights Watch) limewatuhumu walinzi wa mpaka wa Saudi Arabia kwa kutekeleza mauaji ya wahamiaji kwenye mpaka wa Yemen. Anaripoti Mlelwa Kiwale, TUDARCo kwa msaada wa Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Human Rights Watch, mamia ya watu, wengi wao wakiwa ni raia wa Ethiopia waliokuwa na lengo la kuvuka kutoka nchini Yemen inayokumbwa na vita ili kufika Saudi Arabia, wameuawa kwa kupigwa risasi.

Shirika hilo limesema limewahoji wahamiaji 38 raia wa Ethiopia waliojaribu kuvuka kuingia nchini Saudi Arabia wakitokea nchini Yemen pamoja na kuchunguza picha za satellite, video na picha zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii na taarifa kutoka kwa vyanzo vingine.

Ripoti hiyo imesema, baadhi ya walionusurika walieleza kushambuliwa kwa karibu huku walinzi wa mpakani wa Saudi wakiwauliza raia wa Ethiopia wangependelea kupigwa risasi katika kiungo kipi cha miili yao.

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 20 kutoka eneo la Oromia nchini Ethiopia alisema walinzi wa mpaka wa Saudi walifyatua risasi kwenye kundi la wahamiaji waliokuwa wameachiwa kutoka kizuizini.

“Waliturushia risasi kama mvua. Ninapokumbuka, nalia. Nilimwona kijana mmoja akiomba msaada, akapoteza miguu yake yote miwili. Alikuwa akipiga kelele, alikuwa akisema, ‘Unaniacha hapa? Tafadhali usiniache!,” alisema na kuongeza;

“Hatukuweza kumsaidia kwa sababu tulikuwa tunakimbia kwa ajili ya kuokoa maisha yetu,” alieleza zaidi.

HRW iliitaka Saudi Arabia kubadili sera yoyote ya kutumia nguvu dhidi ya wahamiaji na wanaotafuta hifadhi na kuutaka Umoja wa Mataifa kuchunguza madai ya mauaji hayo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoKimataifa

Mwanajeshi amuua mchungaji baada ya kumfuma na mkewe kitandani kwake

Spread the loveHali ya simanzi imetanda katika kijiji kimoja huko Kapsabet kaunti...

Habari za SiasaKimataifa

Mmoja afariki, 30 wajeruhiwa maandamano Kenya

Spread the loveMtu mmoja ameripotiwa kuuawa na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Ramaphosa achaguliwa tena kuwa rais Afrika Kusini

Spread the loveRais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amechaguliwa na wabunge wa...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

DA, ANC waridhia kuunda serikali ya mseto Afrika Kusini

Spread the loveChama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress, ANC,...

error: Content is protected !!