Sunday , 28 April 2024
Home Kitengo Biashara Mchakato kuunganisha Tanga Cement, Twiga Cement wapata kizingiti, Jaji atoa uamuzi
Biashara

Mchakato kuunganisha Tanga Cement, Twiga Cement wapata kizingiti, Jaji atoa uamuzi

Spread the love

BARAZA la Ushindani wa Biashara (FCT) limetoa uamuzi kuhusu uamuzi wa Tume ya Ushindani (FCC) wa kuruhusu kampuni ya Scancem International DA inayomiliki kampuni ya Saruji ya Twiga kununua hisa za Kampuni ya Saruji ya Tanga kupitia uamuzi wake ulioutoa Februari 28, mwaka huu.  Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Uamuzi huo ulifanyika baada ya ule wa awali kukatazwa na FCT Septemba, 2022 baada ya kufunguliwa kwa shauri na baadhi ya wadau kuwa uuzaji wa hisa hizo ambao ungesababisha muunganoko kati ya Twiga Cement na Tanga Cement ungesababisha athari za kibiashara.

Miongoni mwa athari zilizowasilishwa mbele ya baraza hilo na wadau hao ni kuwapo kwa ukiritimba katika soko kutokana na mzalishaji mmoja kuwa na asilimia nyingi na kuwapo kwa uwezekano wa kupanga bei ya bidhaa, hivyo kuathiri watumiaji.

Pamoja na kuwapo kwa katazo la muunganiiko huo, FCC ilitangaza tena kuwa muunganiko huo baina ya kampuni hizo mbili unarejewa na kukaribisha wadau kutoa maoni, jambo ambalo lilisababisha baadhi ya wadau kutaka jambo hilo lizuiwe kisheria na kwamba linakiuka sheria na uamuzi uliotolewa na FCT ambacho ni chombo cha juu katika utatuzi wa migogoro ya kibiashara.

Kutokana na hali hiyo, kampuni ya Saruji ya Chalinze ilikata rufani FCT kupinga uamuzi wa FCC kuruhusu muunganoko huo na baraza hilo limetoa uamuzi unaozuia kuendelea kwa muunganiko huo huku likisisitiza kwamba umezuiwa kisheria.

Katika hoja zake za rufani, mrufani alidai kuwa FCC ilikosea kisheria kwa kuruhusu muunganiko ambao ulikatazwa na FCT katika uamuzi wake uliotolewa Septemba 23, 2022.

Pia FCC ilidaiwa ilikosea kisheria kwa kuitisha upya mchakato wa muunganiko wakati shauri hilo lilishatolewa uamuzi.

Hoja nyigine katika rufani hiyo ni kwamba FCC ilikiuka sheria kwa kudai kuwa katazo la FCT halizuii moja kwa moja, hivyo si la kudumu kwa kuzuia muungano wa kampuni hizo.

Hata hivyo, mjibu rufani namba moja, FCC na Wakili Mkuu wa Serikali ambaye ni mjibu rufani namba mbili, waliibua hoja kwamba mchakato wa Februari, 2023 ulifanyika baada ya kufanya upembuzi yakinifu wa kisoko kuwa hakuna madhara yanayoweza kujitokeza.

Pamoja na hoja hiyo, FCT katika uamuzi wake imesema FCC ilifanya uchunguzi na kutoa ripoti ambayo inaonyesha dhahiri kwamba muunganiko unaokusudiwa unaweza kuwa na athari katika ushindani.

“Baada ya kujiridhisha kuwapo kwa athari za kiushindani na uchumi kama muunganiko huu utapata kibali, mjibu rufani namba moja aliendelea na mchakato …

“Baada ya kufanya tathmini na kuangalia uzito wa hoja, Baraza (FCT) limeridhika kwamba kama muunganiko huu utapitishwa bila masharti yoyote, kuna uwezekano wa kuathiri watumiaji wa bidhaa, hivyo muunganoko huo umezuiwa,” ilieleza sehemu ya hukumu hiyo.

Jaji Maghimbi pia alisema pamoja na kukubaliana na hilo kwamba kuna uwezekano wa kubadilika kwa nguvu za soko, haridhiki na muda mfupi uliotolewa katika kurekewa kwa mchakato.

Kwa mantiki hiyo, alisema haridhiki na mabadiliko hayo ambayo yangelifanya Baraza kurejea uamuzi wake wa awali kuhusu muunganiko huo.

Aidha, Jaji Maghimbi katika uamuzi huo, alieleza kushangazwa na FCC ambayo

imepewa jukumu la kusimamia ushindani kwenye masuala ya kiuchumi kwa maslahi ya watumiaji wa bidhaa, kudharau nguvu za kisheria za Baraza kwa kuendelea na mchakato ambao ulizuiwa kisheria.

“Lazima nisisitize kwamba kitendo kilichofanywa na wajibu rufani hakikuakisi ujumbe chanya kwa umma na kwa wawekezaji wenye nia ya kuwekeza katika nchi yetu kwa

kuitisha upya mchakato katika jambo lililokuwa limezuiwa. Jambo hilo limefanywa kinyume dhidi ya uwapo wa utawala wa sheria,” alisema Jaji Maghimbi.

“Sababu kubwa inayowafanya wawekezaji kuona nchi yetu ni ‘paradiso’ katika uwekezaji ni uwapo wa utawala wa sheria, kuheshimu sheria, kutokuwapo upendeleo na usawa mbele ya sheria. Hili halina budi kuheshimiwa kwa namna yoyote pasipo kumpendelea mwekezaji mmoja kwa sababu inaweza kusababisha madhara hasi.

“Kutokana na sababu zilizotatwa awali, nabatilisha uamuzi wa mjibu rufani namba moja kuhusu muunganiko wa Februari 28, 2023,” alisisitiza.

Jaji Maghimbi aliionya FCC kwamba FCT ni chombo cha juu ni chombo cha juu katika kusimamisha sheria na kutatua migogoro inayojitokezak ibiashara, hivyo inapaswakuheshimu uamizu wa awali wa Septemba 2022 ambao ulikataza muunganiko huo.

Pia Jaji Maghimbi katika hukumu hiyo alimuuliza Wakili Mkuu wa Serikali kama kuanzisha mchakato mpya wa Februari 2023 wakati kuna hukumu ya September 2022 kama ilikuwa njia sahihi na alikiri kuwa haikuwa sahihi kufanya hivyo.

Aidha, katika uamuzi huo, Jaji alitoa amri kwamba FCC iombe marejeo ndani ya siku 30 tangu Julai 6, mwaka huu kama inataka kuanzisha mchakato mpya kitu ambacho mpaka sasa hakijagfanyika na muda umemalizika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Maisha ya kasino ni furaha, cheza Book of Eskimo kujichukulia utajiri 

Spread the love  KUPNGA ni kuchagua, chagua kuwa mshindi kila siku kupitia...

Biashara

Sloti ya Mega Jade kasino njia 10 za malipo unaposhinda

Spread the love  TUNAKULETEA mchezo wa kasino wa kufurahisha sana ambapo unapewa...

Biashara

Orb of Destiny kutoka Meridianbet kasino ushindi kwa njia 14  

Spread the love  ORB of Destiny ni mchezo wa sloti kutoka kwa...

Biashara

Jiandalie Strawberry Cocktail yako nyumbani huku unacheza kasino 

Spread the love  UTAANDAA matunda yako unayotaka kutumia unaweza kutumia Strawberry, Cantaloupe...

error: Content is protected !!