Sunday , 5 May 2024
Home Kitengo Biashara Wakuu wa Majeshi Tanzania, Malawi waipongeza NMB udhamini CDF Trophy
BiasharaMichezo

Wakuu wa Majeshi Tanzania, Malawi waipongeza NMB udhamini CDF Trophy

Spread the love

WAKATI Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Malawi (MDF), Jenerali Jacob Mkunda na Jenerali Vicent Nundwe wakiipongeza Benki ya NMB kwa udhamini mnono na endelevu wa Mashindano ya Gofu ya NMB CDF Trophy, benki hiyo imezihakikishia taasisi hizo kuwa itaendelea kudhamini mashindano hayo, na kuwa siri ya hilo ni mashirikiano bora yaliyopo baina ya NMB na JWTZ. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

NMB ilidhamini mashindano hayo ya Gofu ya Mkuu wa Majeshi (CDF Trophy 2023) kwa kiasi cha Sh. 30 milioni, kufanikisha kuwaleta pamoja wakali wa gofu 228 waliochuana kwa siku tatu kwenye Viwanja vya Gofu Lugalo, kuadhimisha miaka 59 ya kuzaliwa kwa JWTZ Septemba Mosi 1964, washiriki wakitokea JWTZ, MDF na raia kutoka mataifa haya mawili jirani.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda (kushoto), akimkabidhi kombe mchezaji wa timu ya gofu ya Benki ya NMB, Abdallah Gunda, baada kushinda mikwaju ya Net Division C katika mashindano ya ‘NMB CDF Trophy 2023’ yaliyofanyika kwenye viwanja vya gofu Lugalo jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na Benki ya NMB. Kulia ni Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi.

Wakizungumza wakati wa kufunga mashindano hayo na kugawa zawadi kwa washindi, Jenerali Mkunda na Jenerali Nundwe, walikiri kutambua thamani kubwa ya mchango wa NMB na wadhamini wenza katika kufanikisha michuano hiyo, wanayoitumia kama jukwaa huru la kuimarisha afya za washiriki na kubadilishana mawazo ya kujiimarisha Kidiplomasia baina ya Majeshi ya Tanzania na Malawi.

Jenerali Mkunda, aliipongeza Klabu ya Gofu Lugalo (TPDF Lugalo Golf Club) kwa ubunifu wa shindano hilo, lakini akasema wazo hilo la Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo (ambaye ni Mwenyekiti wa Gofu Lugalo), lisingewezekana kirahisi kama sio nguvu na sapoti kubwa ya udhamini mnono wa NMB na kwamba ana furaha baada ya kuhakikishiwa udhamini endelevu kutoka kwa benki hiyo.

“Pongezi za dhati kwako Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo kwa ubunifu wako huu wa CDF Trophy, uliowezesha kutukusanya pamoja JWTZ, MDF na washiriki wa kiraia kwa miaka yote hiyo, ikiwemo miaka nane ya udhamini wa NMB, ambao kama si wao, shindano hili lisingekuwa kubwa na lenye mvuto kama lilivyo.

“Zilikuwa siku nzuri, zilizotuweka pamoja na kutupa muda wa kushirikiana, kujadiliana masuala mbalimbali ya Kimichezo na Kidiplomasia, tunatambua na kuthamini mchango mkubwa wa NMB na wadhamini wenza, nakiri kwamba kama sio nyie, hili lisingewezekana kwa kiwango hiki.

“Tumehakikishiwa udhamini endelevu, niwaambie mnachofanya ni kusapoti jitihada za Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, ambayo inathamini michezo na uthibitisho ni nguvu zake katika michezo yote, ikiwemo Gofu, ambako inajenga uwanja mkubwa jijini Dodoma,” alisema Jenerali Mkunda na kuahidi kuyatumia NMB CDF Trophy kama mazoezi kuelekea Mashindano ya Gofu ya Majeshi ya Dunia, huko San Diego, Marekani baadaye mwaka huu.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda (kushoto), akimkabidhi kombe mchezaji wa timu ya gofu ya Benki ya NMB, Sigfrid Ophishas, baada kushinda katika mashindano ya ‘NMB CDF Trophy 2023’ yaliyofanyika kwenye viwanja vya gofu Lugalo jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na Benki ya NMB. Kulia ni Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi.

Kwa upande wake, Jenerali Nundwe akiwakilishwa na Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Henry Odilo kutoa neno la shukrani, alisema CDF Trophy yamekuwa mashindano makubwa, yenye mvuto na ushindani kutokana na Uratibu mzuri wa TPDF Lugalo Golf Club, zaidi ni kwa sababu ya nguvu ya udhamini mnono wa NMB unaowapa hamasa washiriki kiasi cha kuwa na ushindani mkubwa katika kategori zote.

“Pongezi kwa Waratibu Klabu ya Gofu Lugalo chini ya Mwenyekiti Michael Luwongo na JWTZ kwa ujumla sio tu kwa kuandaa mashindano haya makubwa, bali kutupa nafasi ya sisi kushiriki na aina ya mapokezi tuliyopewa na kuoneshwa kwa siku zote za kuwa hapa.

“Tunawapongeza wadhamini NMB kwa kuipa CDF Trophy thamani kubwa, tunaamini wataendelea kuyadhamini na Gofu Lugalo watazingatia ushiriki wetu kila mwaka, kama ambavyo nasi tutawaalika JWTZ katika mshindano yetu yatakayofanyika Novemba mwaka huu jijini Lilongwe, Malawi,” alisema Jenerali Mstaafu Odilo.

Awali, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi, aliwapongeza waandaaji wa CDF Trophy, washindi wa mwaka huu na washiriki wote kwa ujumla, huku akiihakikishia JWTZ kwamba benki yake itaendelea kuyadhamini mashindano hayo kwa miaka mingi zaidi ijayo, kwani inathamini ushirikiano uliopo baina yao na ndio siri ya kusaidia harakati mbalimbali za kimichezo za Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini.

“Tumedhamimi CDF Trophy kwa miaka nane sasa mfululizo, ahadi yetu kwenu Klabu ya Gofu Lugalo na JWTZ kwa ujumla, tutegemeeni sana sio tu katika suala zima la udhamini wa shindano hili, bali ufadhili wa timu za Majeshi yetu yanapojiandaa na Mashindano ya Majeshi kwa michezo yote, ikiwemo gofu, ngumi, mieleka, riadha, soka na mingineyo ya kitaifa na kimataifa kama ile ya Nairobi, Kenya na Wuhan, China.

“NMB ni mdau mkubwa wa JWTZ, taasisi ambayo Ina wateja wetu wengi na hiyo ndio siri ya kujitoa kwetu kuwezesha shughuli za kimichezo majeshini. Tunawahakikishia pia huduma bora na rafiki kwa ajili yenu, zinazotolewa kwenye matawi yote, yakiwemo matawi maalum ya Mlimani City, Tegeta, Ohio na Oyster Plaza,” alisema huku alizitambulisha bidhaa mbili mpya za Akiba Plus na Wezesha Account.

Mshindi wa jumla wa mashindano ya gofu ya NMB CDF Trophy 2023, Michael Massawe (katikati), akionesha zawadi alizokabidhiwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob Mkunda (wa pili kushoto), wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi iliyofanyika kwenye viwanja vya gofu Lugalo jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Kulia ni Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi na wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Klabu ya Gofu Lugalo, Brigedia Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Michael Luwongo.

Kwa upande wa matokeo, Michael Massawe aliibuka mshindi wa jumla wa CDF Trophy 2023, huku Abdallah Yusuf akitwaa taji upande wa wachezaji wa kulipwa ‘professional,’ wakati Abdallah Gunda wa NMB akiibuka bingwa wa mataji mawili katika ‘Sponsors Category,’ na ‘Division C’. Naye Sigfrid Urassa wa NMB, pia aliibuka na vikombe viwili vya ‘Men’s Smart Golfers’ na mshindi wa pili ‘Sponsors Category’.

Baadhi ya washindi wengine na kategori zao kwenye mabano ni: Amina Khamis (Combat Fiddle – ladies), David Mziray (Combat Fiddle – men’s), Private Lawrence Sangawe (Division B), Vicky Elias (Ladies), Mtei Mwamapala (men’s longest drivers), Loveness Konky (ladies longest drivers) na Prosper Emmanuel (Division A).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Usiishie kuangalia tu game za leo, piga na mkwanja na Meridianbet

Spread the love  LIGI mbalimbali barani ulaya zitarejea tena Jumamosi ya leo...

Biashara

Pata Mil 450 ya Non Stop Drop ukicheza Meridianbet kasino

Spread the love  JIUNGE na promosheni ya Kusisimua iitwayo NON-STOP DROP, inayotolewa...

Biashara

Exim Bank yaendeleza malipo ya kidijitali na Chef’s Pride Dodoma

Spread the love  BENKI ya Exim imeingia makubaliano na Mgahawa wa Chef’s...

Michezo

Ligi mbalimbali za pesa kuendelea leo

Spread the love Ijumaa ya leo ambapo mechi mbalimbali zinaendelea Duniani Meridianbet...

error: Content is protected !!