Tuesday , 5 December 2023
Home Kitengo Biashara Wajasiriamali waitwa maonyesho Burundi
Biashara

Wajasiriamali waitwa maonyesho Burundi

Spread the love

MWENYEKITI wa Shirikisho la Wajasiriamali wa Jumuiya ya  Afrika Mashariki, Josephat Rweyemamu ametoa wito kwa wanachama shirikisho hilo kushiriki kwa wingi kwenye maonyesho ya wajasiliamali JUAKALI Nguvu Kazi Afrika Mashariki yatakayofanyika nchini jijini Bujumbura nchini  Burundi, kuanzia Desemba 5 hadi 15 mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Rweyemamu ametoa wito huo leo  jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo ambapo ameweka wazi kuwa jumuiya hiyo ilianza mwaka 1999 baada ya kurejeshwa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kwamba maonesho hayo yanafanywa kwa kuzunguka nchi wanachama.

“Maonyesho haya ni ya 23 tangu kuazishwa kwake na katika maonyesho haya zitafanyika shughuli mbalimbali, kutakuwa na siku ya Tanzanaia ambayo itafanyika Disemba 10  na itakuwa siku mahususi ya kuonyesha bidhaa zetu,”amesema

Amesema kuwa wameshatoa fomu kwa ajili ya wajasiriamali wanaotaka kushiriki wajaze na kuzirudisha mapema kwa  kuzingatia muda, huku akitarajia Tanzania kuwakilishwa na washiriki 300 ambao watakuwa na bidhaa mbalimbali za kusindika, nguo na nyinginezo.

Ameongeza kuwa maonyesho hayo yanatarajiwa kuwa na wajasiriamali 1000 kutoka nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwemo Sudan Kusini, DR Congo, Rwanda,  Burundi, Kenya, Uganda na Tanzania na kauli mbiu ya mwaka huu ni “Kuwaunganisha wajasiliamali wadogo na kati wa Afrika Mashariki kufanya biashara katika eneo la jumuiya hiyo”

Rweyemamu amesema  maonyesho hayo yanafundisha wafanyabiashara namna ya kuvuka mipaka na kujua sheria na taratibu.

Mwenyekiti amesema pia wanahamasisha vijana kushiriki kwa wingi ili kuweza kuingia kwenye ujasiriamali wakiwa vijana kwa lengo la kuongeza ubunifu .

Amesema  maonyesho hayo ni fursa hivyo nivema watu wakajiandikisha kwa wingi, ili kuweza kushiriki na kuweza kujifunza kwa wenzao ambao wamepiga hatua kwenye eneo hilo.

Rweyemamu amewataka washiriki kuzingatia taratibu zote za kusafiri nje ya nchi ikiwemo hati ya kusafiria, kuchanga korona, gharama za kubadilisha fedha na mengine.

Naye Mratibu Mkuu wa Maonesho hayo ya JUAKALI Nguvu Kazi,  Zubeda Omar amewataka wajasiriamali kujitokeza kuchukua fomu na kwenda  kushiriki na kuachana na tabia ya kulalamika kwamba hawapewi fursa.

Zubeda amesema mwitikio wa kujaza fomu za ushiriki ni mkubwa na matumaini yao ni kuona ushiriki wa Watanzania ukiwa na tija.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaMichezo

Mwana FA anogesha Tamasha la Exim Bima Festival

Spread the loveNAIBU Waziri Wa Utamaduni, Sanaa Na Michezo, Hamis Mwinjuma ‘Mwana...

Biashara

Haya ni Maajabu ya sloti ya Jade Valley ya kasino ya mtandaoni Meridianbet

Spread the love  JADE Valley ni mchezo wa sloti wenye nguzo tano...

Biashara

Washindi wa Serengeti Maokoto ndani ya Kizibo Dar, Dodoma walamba mzigo

Spread the love Mustapha Ally, Mkazi wa Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma...

Biashara

Shinda mtonyo mrefu ukicheza Shaolin Crew kasino ya  Meridianbet

Spread the love  TAIFA la Uchina limebebwa na historia kubwa sana, wengi...

error: Content is protected !!