Monday , 11 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Sangu aipa kongole SumaJKT kwa miradi
Habari Mchanganyiko

Sangu aipa kongole SumaJKT kwa miradi

Spread the love

MWENYEKITI wa Kamati ya  Kudumu ya Bunge na Uwekezaji wa Mitaji ya Umma na Mbunge wa Kwela, Deus Sangu  amepongeza kamati hiyo kwa kufanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali inayoendeshwa na Kampuni ya SUMAJKT ya uzalishaji mali. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Amesema kipekee wamepata fursa ya kutembelea sehemu kuu mbili kwanza wametembelea Kampuni tanzu ya uzalishaji jwa maana ya uzalishaji nguo pia kampuni tanzu nyingine ya uzalishaji maji na kikubwa nikuendelea kuipongeza Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwanamna ambavyo ameiwezesha SUMAJKT katika uwekezaji.


Sangu ameyasema hayo tarehe 15  Novemba mwaka huu jijini Dar es Salaam,  ambapo ambapo kamati hiyo  imejionea kiwanda cha nguo ambacho kimewekeza fedha takribani  milioni 361…

Mbunge huyo amesema kampuni hizo zimefanya  kazi kubwa na Serikali inastahili pongezi, huku akizitaka kuendelea na uzalishaji kwa kasi.

“Uwekezaji huu umeweza kuongeza uzalishaji, mwanzo kiwanda kilikuwa na uwezo wa kuzalisha nguo 350 lakini  umeongezeka na sasa wanazalisha pisi 500 na bado wanahitaji kupewa nguvu zaidi na sapoti ili waweze kuzalisha pisi 1,000 kwa siku na kwakweli tunaona namna walivyojipanga na idadi ya wateja imeongezeka hadi nje ya nchi,” amesema Mbunge Sangu

Amesema SUMAJKT wametoa fursa ya ajira kwa vijana wakitanzania takribani 350 wakiwa ni askari na raia wa kawaida ambao ni asilimia 70.

Kwa upande mwingine amepongeza uamuzi wa SUMAJKT kuwekeza takribani Shilingi bilioni 1 832 kwenye uzalishaji wa chapa za maji kutoka chupa 3,200 hadi 10,000 na kwamba wataendelea kushauri serikali iongeze mtaji zaidi.

Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali, Rajabu Mabele amesema wanampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufanya mahusiano ya kidiplomasia ambayo yameweza kuwasadia kupata soko la bidhaa zao hadi nje ya nchi.

Alisema mikakati yao ni kuhakikisha miradi wanayosimamia inachangia ukuaji wa uchumi wa nchi

“Kulikuwa na laini mbili za uzalishaji lakini sasa hivi tunalaini sita na uzalishaji wa kuzalisha nguo 300 kwa siku, hivi sasa tunazalisha nguo 700 na lengo letu nikuelekea katika kuzalisha nguo 1,000 kwa siku kwa hiyo bado tunaendelea kuzalisha na masoko kiukweli tunamshukuru sana Rais Samia kwa kuendelea kutanua wigo katika diplomasia ya uchumi kwani mahusiano na nchi nyingi ni mazuri,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Kesi ya mfanyakazi wa CRDB itaendelea J’tatu

Spread the love  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam inatarajia...

Habari Mchanganyiko

Mawasiliano Dar – Bagamoyo yarejea

Spread the loveMAWASILIANO ya barabara ya Mkoa wa Pwani na Dar es...

Habari Mchanganyiko

Tanesco: Mvua chanzo kukatika umeme leo

Spread the loveShirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limedai kuwa hitilafu iliyojitokeza katika...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Zara tours yajivunia kupandisha wageni 228 Mlima Kilimanjaro

Spread the loveKampuni ya utalii ya Zara tours ya mjini Moshi mkoani...

error: Content is protected !!