Wednesday , 6 December 2023
Home Kitengo Maisha Afya Wagonjwa kiharusi waongezeka, Hospitali Mkapa yaja matibabu mapya
AfyaHabari Mchanganyiko

Wagonjwa kiharusi waongezeka, Hospitali Mkapa yaja matibabu mapya

Spread the love

HOSPITALI ya Benjamini Mkapa kwa kushirikiana na madaktari Bingwa kutoka nchi Japan kupitia taasisi ya Tokushikai Medical group ya Japan wanatarajia kuanzisha huduma ya matibabubu ya ubongo bila  upasuaji wa  kufungua fuvu. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma …(endelea).

Hayo yameelezwa janaJumatatu tarehe 2 Oktoba 2023 na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamini Mkapa,Dk. Alphonce Chandika alipozungumza na waandishi wa habari juu ya kuanzishwa kwa huduma hiyo muhimu.

Mkurugenzi mtendaji wa BMH Dk.Alphonce Chandika akizungumza na waandishi wa habari juu ya uanzishwaji wa huduma ya kutibu ubongo bila kufunua fuvu.


Dk.Chandika amesema huduma hiyo ambayo ni kwa nadra kuipata nchini na wakati mwingine kwenye mataifa ya nje kwa sasa itapatikana nchini Tanzania na kwenye hospitali ya Benjamini Mkapa.

Mbali na kupatikana kwa huduma hiyo hapa nchini itasaidia kuharakisha upatikanaji wa matibabu na kuokoa gharama ya kutibiwa nje.

Amesema asilimia kubwa ya watanzania wanakutwa na matatizo kwenye ubongo ambayo unasababishwa na damu kuganda ndani ya mishipa ya kusukuma damu kwenye ubongo na kusababisha mtu kupata kiarusi.

Aidha, amesema wagonjwa ambao hupata matibabu kwa kufumuliwa fuvi la kichwa utumia muda mrefi kupona na kuchukua muda mrefu kwa kuwekwa kwenye chumba mahututi.

Akizungumzia ushirikiano wa Hospitali ya Benjamini Mkapa na madaktari bingwa kutoka nchini Japan amesema hatua hiyo ni utekelezaji wa  juhudi za Serikali katika kujali afya za watanzania.

Dk. Chandika amesema kwa sasa wanaendelea na mafunzo na kupata uzoefu wa kutumia mashine ambazo ni za kisasa ambazo zinafanya kazi ya kuzibua mishipa ndani ya ubongo bila kufumua fuvu.

Daktari bingwa wa upasuaji wa mifupa ya fahamu,uti wa Mgongo na ubongo,Dk.Henry Humba,akizungumzia hali ya ugonjwa wa ubongo nchini

Kwa upande wake Daktari bingwa wa upasuaji wa mifupa ya Fahamu,uti wa Mgongo na ubongo, Dk.Henry Humba,amesema ongezeko la wagonjwa wa kiharusi ni kubwa nchini huku akielezea kuwa Hospitali ya Benjamini Mkapa kwa wiki inapokea wagonjwa kati ya wanne hadi watano.

Hata hivyo, amesema asilimia ya 60 ya watu wanaopata kiharusi hutokana na kuziba kwa mishipa ya damu ambayo inaingia kwenye ubongo.

Akizungumzia uzoefu wa kutumia mashine za kisasa za kutoa huduma ya kutibu ubongo bila kufunua fuvu amesema inatakiwa kufanya mazoezi ndani ya mwaka mmoja ili kupata mafunzo ya kutosha kwa kutoa hiyo huduma.

Akizungumzia juu ya wataalamu amesema kuwa nchi nzima ina wataalamu wapatao 28 tu jambo ambalo ni wachache hivyo kuna haja ya kuhakikisha wanapata mafunzo kwa kushirikiana na wataalamu kutoka nchini Japani

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

RAS Songwe: Tumepigwa… mkurugenzi nakupa siku 21

Spread the loveKATIBU tawala mkoani Songwe, Happines Seneda ametoa siku 21 kwa...

Habari Mchanganyiko

Shura ya Maimamu kukata rufaa kupinga Sheikh kufungwa miaka 7

Spread the loveSHURA ya Maimamu Tanzania, inakusudia kukata rufaa dhidi ya hukumu...

Habari Mchanganyiko

TMA yaagizwa kutangaza mafanikio yao kikanda, kimataifa

Spread the love  KATIBU Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara ameiagiza...

Habari Mchanganyiko

NMB yasaidia waathirika wa mafuriko, maporomoko Hanang

Spread the loveWaathirika wa maporomoko ya tope Wilayani Hanang, mkoani Manyara, waliopoteza...

error: Content is protected !!