Thursday , 7 December 2023
Home Kitengo Maisha Afya Chanjo mpya ya malaria Sh 5,000-10,000
AfyaHabari Mchanganyiko

Chanjo mpya ya malaria Sh 5,000-10,000

Spread the love

Shirika la afya la Duniani (WHO) limeridhia chanjo ya pili ya ugonjwa wa malaria kwa watoto ambayo inaweza kuokoa maisha ya maelfu ya watoto endapo kutakuwapo usambazaji wa kutosha. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea)

Takriban watoto 500,000 katika ukanda wa Afrika hufariki kila mwaka kutokana na ugonjwa huo unaosababishwa na vimelea vinavyoenezwa na mbu.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, Tedros Ghebreyesus amenukuliwa akiseama “Kama mtafiti wa malaria, nilikuwa na ndoto ya siku ambayo tutakuwa na chanjo salama na yenye ufanisi dhidi ya malaria. Sasa tunazo mbili.”

Chanjo mpya ya R21/Matrix-M, iliyotengenezwa na Chuo Kikuu cha Oxford cha Uingereza na kuzalishwa na taasisi ya Serum ya India, tayari imeidhinishwa kutumika nchini Burkina Faso, Ghana na Nigeria.

Dozi ya R21/Matrix-M inagharimu kati ya Dola mbili hadi nne za Marekani sawa na Sh 5,000 hadi 10,000.

Mwaka 2021, chanjo ya RTS,S, iliyotolewa na kampuni kubwa ya dawa ya Uingereza GSK, ilikuwa ya kwanza kupendekezwa na WHO katika kudhibiti ugonjwa wa malaria kwa watoto katika maeneo yenye maambukizi ya wastani hadi ya juu.

Tedros amesema kumekuwa na uhitaji mkubwa wa chanjo ya RTS,S, kwa hivyo chanjo hii ya sasa ya nyongeza itakuwa hatua muhimu katika kuwalinda watoto kwa haraka zaidi, na itawaleta pamoja katika ile dira ya kutokomeza kaibsa malaria.

Tangu mwaka 2019, mipango ya majaribio ya kuanzisha chanjo ya RTS,S katika nchi tatu — Ghana, Kenya na Malawi — imewezesha watoto milioni 1.7 kupata angalau dozi moja. Mipango hii imesababisha kupungua kwa kiasi kikubwa kwa aina kali na mbaya za malaria, na kupunguza kwa vifo vya watoto.

WHO imesema angalau nchi 28 za Afrika zinapanga kuanzisha matumizi ya chanjo hiyo mpya ya malaria iliyopendekezwa ikiwa kama sehemu ya programu zao za kitaifa za chanjo.

Imesema chanjo ya RTS,S itapelekwa katika baadhi ya nchi za Afrika mapema 2024, na chanjo ya R21 inatarajiwa kupatikana katikati ya 2024.

Chanjo hizi mbili zina viwango sawa vya ufanisi vya karibu asilimia 75.

Taarifa wa wadau wa chanjo inasema WHO na washirika wake wametoa maombi ya dozi milioni 60 ifikapo mwaka 2026. Kiwango hicho kinatarajiwa kuongezeka na kufikia dozi milioni 100 ifikapo 2030.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

RAS Songwe: Tumepigwa… mkurugenzi nakupa siku 21

Spread the loveKATIBU tawala mkoani Songwe, Happines Seneda ametoa siku 21 kwa...

Habari Mchanganyiko

Shura ya Maimamu kukata rufaa kupinga Sheikh kufungwa miaka 7

Spread the loveSHURA ya Maimamu Tanzania, inakusudia kukata rufaa dhidi ya hukumu...

Habari Mchanganyiko

TMA yaagizwa kutangaza mafanikio yao kikanda, kimataifa

Spread the love  KATIBU Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara ameiagiza...

Habari Mchanganyiko

NMB yasaidia waathirika wa mafuriko, maporomoko Hanang

Spread the loveWaathirika wa maporomoko ya tope Wilayani Hanang, mkoani Manyara, waliopoteza...

error: Content is protected !!