Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Biashara NBC yazindua mwezi wa huduma kwa wateja kwa kuwatembelea mawakala, wateja
Biashara

NBC yazindua mwezi wa huduma kwa wateja kwa kuwatembelea mawakala, wateja

Spread the love

Benki ya Taifa ya Biashara – NBC imetumia maadhimisho ya mwezi wa huduma kwa wateja kwa kuwatembelea mawakala mbalimbali na wateja wa benki hiyo katika maeneo mbalimbali ili kuthibitisha na kutambua thamani na mchango wa wadau hao muhimu katika kuwahudumia wateja na ukuaji wa uchumi kwa ujumla. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Zoezi hilo la kuwatembelea wadau hao limefanyika mapema leo Jumanne jijini Dar es Salaam likihusisha wafanyakazi wakiongozwa na viongozi waandamizi wa benki hiyo akiwemo Mkuu wa Uendeshaji NBC, Alelio Lowassa, Mkuu wa Kitengo cha Compliance NBC, Sarah Laiser, Mkuu wa Kitengo cha Uwakala, Gaudence Shawa na Mkurugenzi wa Wateja wadogo na Binafsi wa Benki ya NBC, Elibariki Masuke aliyemuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi.

Mkurugenzi wa Wateja wadogo na Binafsi wa Benki ya NBC Elibariki Masuke akizungumza na wafanyakazi, mawakala wakubwa na wadogo wa benki hiyo wakati viongozi na wafanyakazi wa benki hiyo walipotembelea wakala mkuu wa benki hiyo eneo la Goba, jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya mwezi wa huduma kwa wateja wa benki hiyo.

Akizungumza kwenye tukio hilo lililohusisha maeneo ya Goba, Sinza na Tandale, Masuke alisema hatua ya benki hiyo kuelekeza maadhimisho hayo kutambua zaidi mchango wa mawakala wa benki hiyo ni kutokana na kuthamini kazi kubwa inayoendelea kufanywa na mawakala hao katika kuwahudumia wateja kwa ukaribu, uaminifu na kwa weledi wa hali juu.

“Tumeona tuyatumie maadhimisho haya kwa kuwatembelea mawakala wakuu sambamba na baadhi ya mawakala wadogo bila kuwasahau wateja wetu ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wao muhimu kwa ustawi wa benki na uchumi kwa ujumla na hiyo ndio sababu kauli mbiu yetu ni NBC Timu Huduma kwasababu huduma zetu tunazitoa kama timu.’’

“Mawakala hawa wameonyesha weledi,uaminifu wa hali ya juu na hivyo wamekuwa wakitoa huduma kwa ukaribu zaidi hata katika maeneo ambayo matawi yetu hayajafika tena kwa viwango vilevile kama ambavyo tunatoa huduma kwenye matawi yetu mengine. Hivyo tumeona wanastahili heshima hii sambamba na zawadi mbalimbali ambazo tumewapatia hii leo tukilenga kuwahamasisha na kuwahimiza kufanya vyema zaidi katika majukumu yao. ,’’ alibainisha.

Mkuu wa Kitengo cha Compliance NBC, Sarah Laiser, (kushoto) akimkabidhi zawadi mmoja wa wakala mkuu wa benki hiyo, Christian Makawa (wa tatu kushoto) wa eneo la Tandale, jijini Dar es Salaam ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa huduma zinazotolewa na wakala huyo kwa wateja wa benki hiyo na ukuaji wa uchumi kwa ujumla.

Kwa mujibu wa Masuke pamoja na mtandao mpana wa takribani mawakala 12,000 wa benki hiyo kote nchini, bado benki hiyo inaendelea na mkakati wake wa kufungua matawi mapya katika maeneo mbalimbali nchini ili kurahisisha huduma kwa wateja na mawakala hao.

Akizungumza na baadhi ya wateja waliotembelewa na benki hiyo Mkuu wa Kitengo cha Compliance NBC, Sarah Laiser aliwashukuru wateja hao kwa kuendelea kuiamini benki hiyo huku akiahidi kuendeleza ushirikiano huo sambamba na kubuni huduma mbalimbali zinazolenga kurahisisha huduma zinazotolewa na wateja hao zikiwemo huduma za malipo.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Benki ya NBC, Salama Mussa aliwashukuru mawakala na wateja wa benki hiyo kwa mchango wao katika kufanikisha ustawi wa benki hiyo sambamba na kupongeza ustawi wa biashara zao kufuatia huduma za kisasa zinazotolewa na benki hiyo.

Aliahidi kwa niaba ya benki hiyo kuendelea kutoa huduma bora zitakazokidhi mahitaji ya wakati uliopo na ujao wa wateja na mawakala hao.

Kwa upande wao Mawakala na wateja waliotembelewa walitoa shukrani zao za dhati kwa huduma na ushirikiano unaoendelea kutolewa na benki hiyo huku wakiipongeza benki hiyo kwa namna inavyeondelea kubuni huduma zinazolenga kutatua changamoto za wateja sambamba na kuwapatia elimu ya mara kwa mara inayolenga kuwajengea uwezo katika kutumia huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo.

“Imekuwa ni heshima kubwa kwetu kwa kutambuliwa na Benki ya NBC. Utambuzi huu unatupa motisha ya kufanya kazi nzuri zaidi kwa wateja wetu, kuhakikisha tunawapa huduma bora iwezekanavyo.

Zaidi tunawashukuru sana NBC kwa huduma zao kwetu sisi mawakala wakuu ikiwemo huduma ya ulinzi masaa 24, huduma ya kuongeza mitaji yetu yaani ‘Wakala boost’ sambamba na mafunzo mbalimbali kuhusu huduma zao ikiwemo huduma ya Bima” alisema Beatrice Shayo, Wakala Mkuu wa benki hiyo, eneo la Goba.

Naye mmoja wa wateja wa benki hiyo, Jacquelene Madili Mkurugenzi wa duka la vifaa vya nyumbani la Jaden Home Store aliishukuru benki hiyo kwa huduma zake kwa wateja huku akionyesha kuvutiwa na huduma ya malipo ya POS inayotolewa na benki hiyo kutokana na namna inavyorahisisha huduma za duka hilo kwa wateja wake

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Cheza sloti ya Zombie Apocalypse na ushinde kirahisi

Spread the love Wengi wetu hupenda filamu za Mazombie huwa zinatishakidogo lakini...

Biashara

Ushirikishwaji wa wafanyakazi ni muhimu katika utekelezaji wa sera za afya na usalama kazini

Spread the love  KILA ifikapo Aprili 28 ya kila mwaka, dunia huadhimisha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Biashara

Wazir Jr kinara wa ufungaji KMC FC ajiunga Meridianbet

Spread the love    MUITE Wazir Jr ‘The King of CCM Kirumba’,...

error: Content is protected !!