Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wananchi waamua kujenga zahanati kukwepa adha kufuata huduma mbali
Habari Mchanganyiko

Wananchi waamua kujenga zahanati kukwepa adha kufuata huduma mbali

Spread the love

WANANCHI wa Kijiji cha Kwikerege, kilichopo katika Jimbo la Musoma Vijijini, mkoani Mara, wameamua kujenga zahanati yao ili kuepuka aza ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya katika vijiji jirani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mara…(endelea).

Tarehe 1 Oktoba 2023, Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo, aliendesha harambee ya kuchangisha fedha na vifaa kwa ajili ya ujenzi huo, ambapo wananchi wengi wamejitokeza kushiriki kwa kutoa nguvu kazi na matofali.


Katika harambee hiyo, Prof. Muhongo alichangia mifuko ya saruji 100, huku akitoa wito kwa wadau wengine kuunga mkono juhudi hizo za wananchi ambao wameshaanza shughuli za kuchimba msingi na kujenga kwa nguvu zao.

“Kijiji hiki hakiuna zahanati, kwa hiyo wakazi wake wanapohitaji huduma za afya wanalazimika kutembea umbali usiopungua kilomita tani kwenda kwenye zahanati ya jirani ya Kijiji cha Rusoli. Hivyo, wananchi wameamua kujenga zahanati ya kijiji chao,” alisema Prof. Muhongo na kuongeza:

“Mimi natanguliza mifuko 100 kuendana na kasi yenu, halafu wengine huko wataendelea kuchangia kulingana na kasi yenu, mnatakiwa muende kasi.”

Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kwikerege, Mganga Majura, alisema wananchi wake wamechukua hatua hiyo baada ya kuteseka kwa muda mrefu kufuata huduma ya afya mbali, kitendo kinachohatarisha usalama wa maisha yao hasa kina mama wanaojifungua.

Jimbo la Musoma Vijijini lina hospitali moja ya halmashauri yenye hadhi ya wilaya, vituo vya afya sita na zahanati 28 huku zingine 16 zikiwa zinaendelea kujengwa kwa nguvu za wananchi kwa msaada wa Serikali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!