Monday , 11 December 2023
Home Kitengo Biashara BetPawa kuwasaidia Watanzania 20 awamu ya 2 ‘Dream Maker’
BiasharaMichezo

BetPawa kuwasaidia Watanzania 20 awamu ya 2 ‘Dream Maker’

Spread the love

KAMPUNI  ya michezo ya kubahatisha ya BetPawa Tanzania,  jana Jumatatu imezindua awamu ya pili ya programu yake ya kuwasaidia Watanzania wenye mawazo chanya kutimiza ndoto zao inayojulikana kama ‘Dream Maker’. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Meneja Masoko wa Kampuni ya michezo ya kubashiri ya BetPawa Tanzania Borah Ndanyungu (kulia) akimwonyesha mwandishi wa Mwananchi Hellen Hartley namna ya kushiriki kutuma wazo la mradi wakati wa uzinduzi wa Programu ya Dream Maker awamu ya pili iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam. Kupitia programu Watanzania 20 wataweza kusaidiwa kutimiza ndoto zao kwa ufadhili wa BetPawa.

Kupitia awamu ya pili ya programu hiyo, jumla ya Watanzania 20 wenye mawazo ya miradi yenye uwezo wa kubadilisha maisha yao na jamii inayowazunguka, watashikwa mkono na BetPawa na hivyo kutimiza ndoto zao.

Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa msimu wa pili, Meneja masoko wa BetPawa Tanzania, Borah Ndanyungu alisema programu hiyo itahusisha mikoa mitatu ambayo ni Lindi, Mtwara na Ruvuma.

Wafanyakazi wa kampuni ya michezo ya kubashiri ya BetPawa Tanzania wakifurahi katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya uzinduzi wa programu ya Dream Maker awamu ya pili. Kupitia program hiyo ambayo ni sehemu ya kurudisha kwa jamii, Watanzania 20 wataweza kusaidiwa kutimiza ndoto zao kwa ufadhili wa BetPawa.

“Watu watakaokutana na basi maalum la Dream Maker watakaribishwa kupanda na kujaza form pamoja na kurekodi video kuhusu ndoto zao.

“Wengine ambao hawatapata fursa ya kukutana na basi, wanaweza kufanya hivyo popote pale walipo na kutuma kwa njia ya mtandao kwa kutumia hastag #betPawaDreamMaker,” alifafanua

Kwa mujibu wa BetPawa Tanzania, msimu wa kwanza wa Dream Maker uliofanyika Septemba 2021, uliwezesha ndoto za Watanzania 13 kutimizwa.

Ndoto hizo ni pamoja na ujenzi wa nyumba mpya, viwanja vya michezo ufunguzi wa biashara mpya ambazo pia zimetengeneza ajira kwa jamii inayozizunguka. Mwaka huu, jumla ya miradi 20 itapata ufadhili.

Borah alieleza kuwa fursa ipo wazi kwa kila Mtanzania mwenye umri wa miaka 18 na kuendelea na kuwataka wote wenye mawazo ya miradi kujitokeza na kuyawasilisha kwa BetPawa.

“Tunafanya ubashiri kuwa rafiki zaidi kwa kuwapa watu fursa ya kubashiri kwa dau dogo na kushinda kikubwa kisha kutimiza ndoto zao. Hata hivyo, katika programu hii ya Dream Maker, huhitaji kubashiri kabisa kwa kuwa ni ya kila mtu mwenye umri wa miaka 18 au zaidi. “Tueleze ndoto yako bila kujali ukubwa wake. na sisi tutakusaidia kuitimiza na kukufanya kuwa mmoja kati ya wanufaika 20 wa msimu wa pili,” alifafanua Borah

Aliongeza kuwa BetPawa itatembelea mikoa hiyo mitatu na magari ya matangazo yatakuwa yakihamasisha watu kujitokeza na kuelezea ndoto zao. Zoezi hili litafanyika katika mikoa tofauti tofauti kila msimu hadi litakapomaliza nchi nzima

“Lengo la BetPawa Tanzania ni kutoa fursa kwa kila Mtanzania kutimiza ndoto yake,” aliongeza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Pesa ipo huku Meridianbet, beti sasa

Spread the love  WIKIENDI inaishia leo hii jaman kama bado hujasuka mkeka...

Biashara

Meridianbet yatoa msaada Mwenge

Spread the love  KAMPUNI ya Meridianbet imefika maeneo ya Mwenge jijini Dar-es-salaam...

Biashara

Serengeti yakabidhi mkwanja kwa mshindi wa Maokoto ndani ya Kizibo

Spread the love Mshindi wa Maokoto ndani ya kizibo kutoka Kahama Mjini...

Biashara

Ushindi rahisi unpatikana kila ukicheza kasino ya Hot Joker

Spread the love  HOT Joker Fruits 20 ni mchezo wa sloti ya...

error: Content is protected !!