Tuesday , 7 May 2024
Home Kitengo Biashara   Wachimbaji dhahabu Kahama waunda ushirika, wapewa ujumbe mzito
Biashara

  Wachimbaji dhahabu Kahama waunda ushirika, wapewa ujumbe mzito

Spread the love

WACHIMBAJI wa madini ya dhahabu wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuwa mstari wa mbele kwa kushirikiana na Serikali katika kutatua changamoto mbalimbali ambazo zinazorotesha utendaji wao. Anaripoti Paul Kayanda, Shinyanga …(endelea).

Wito huo umetolewa na Mrajisi msadizi wa Vyama vya ushirika Mkoa wa Shinyanga, Hilda Bonifasi wakati  akizindua Mkutano Mkuu wa Kwanza  wa uchaguzi wa Ushirika wa pamoja wa Wachimbaji madini  ya dhahabu (KAMIKOJE) ulifanyika leo tarehe 13 Juni 2023 wilayani hapa.

Mrajisi msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga, Hilda Boniphace akizungumza baada ya uchaguzi huo wa kumpata mwenyekiti wa Kamicoje Wilaya ya Kahama.


Bonifasi mesema umoja huo ambao unajumuisha vyama vya Igomico, Kamicoso, Bms, Kamicos na Mkamico anawapongeza  kwa kufikia hatua ya kuunda ushirika kwani ni hatua kubwa ambayo wamefikia.

Amesema umoja huo utalenga katika kutatua changamoto ambazo zitakuwa zikiwakabili wachimbaji hao.

Amesema cheti ambacho atawapa ni kuutambulisha mradi huo wa pamoja wa wachimbaji wa dhahabu waliopo.

Aidha, Bonifasi amewataka maofisa ushirika kuendelea kutoa elimu ya ushirika kwa wachimbaji wa madini ya dhahabu kila siku ili kuhakikisha kuwa wanaufahamu ushirika kwa hali ya juu ili kuwepo na mabadiliko katika sekta hiyo ya madini.

Amesema uchaguzi wa viongozi wa ushirika huo utazingatia misingi ya kisheria  kwani taasisi hiyo iliyoanzishwa ni kubwa inaweza kuitwa popote pale hivyo viongozi watakaochaguliwa lazima wawe watu wanaojielewa na wenye kipaji cha uongozi.

Amewataka wote watakaochaguliwa wapewe semina elekezi za uongozi ili kupata uwezo wa kuweza kuwaongoza wanachama.

Amesema atahamasisha wachimbaji wengine katika maeneo mbalimbali ya uchimbaji Mkoa wa Shinyanga kuhakikisha kuwa wanaunda ushirika kama huu uliopo.

Katika uchaguzi huo ambao ulijumuisha wagombea 10 wakiwemo wajumbe wa Bodi, Asha Msangi alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa ushirika huo huku makamu mwenyekiti akiwa Cosmas Paul ambao kwa mujibu wa sheria watatakiwaa kuongoza kwa kipindi cha miaka mitatu.

Aidha, Mwenyekiti mpya wa Bodi mpya ya Kamicoje, Asha Msangi amewashukuru wanachama kwa kuonesha kumuamini katika kuongoza bodi hiyo kwani wanawake wengi  hawaaminiwi katika nafasi za uongozi.

Amesema kuwa atahakikisha anawaunganisha wachimbaji wa dhahabu na kuongeza kuwa yeye ni kiongozi anayefanya kazi katika mstari ulionyooka kama atapata ushirikiano kutoka kwa wanachama ambao ndio waliomweka madarakani kwa kipindi cha miaka hiyo mitatu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

Biashara

Cheza kwa kuanzia Sh 400 kushinda mgao wa Expanse Tournament kasino 

Spread the love  UKISIKIA bosi kacheka ujue Maokoto yanafuatia, Kupitia promosheni pendwa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Biashara

Mchezo wa maokoto Cobra Queen unapatikana Meridianbet

Spread the love Meridianbet Kasino Mtandaoni utapata fursa ya kufurahiamchezo uliochochewa na...

error: Content is protected !!