Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wabunge wapokea maoni yaliyoachwa kwenye muswada wa habari
Habari Mchanganyiko

Wabunge wapokea maoni yaliyoachwa kwenye muswada wa habari

Spread the love

 

BAADHI ya wabunge wameanza kupokea mapendekezo ya wadau wa habari yaliyoachwa katika Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Huduma ya Habari ya 2016. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma …(endelea).

Wabunge wameanza kupokea mapendekezo hayo jana tarehe 24 Aprili 2023, kutoka kwa wajumbe wa Wadau wa Haki ya Kupata Habari (CoRI), jijini Dodoma.

Mbunge wa Mlalo, Rashid Shangazi (CCM) ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, ameahidi kushirikiana na wadau wa habari katika kuhakikisha mapendekezo yaliyoachwa katika muswada huo yanafanyiwa kazi, huku akibainisha kwamba baadhi ya mapendekezo yaliyoingizwa katika Muswada huo yana ukakasi.

Shangazi aliahidi kushirikiana na wadau wa habari katika kuhakikisha sheria hiyo inaboreshwa kwa kuondolewa vifungu vyenye dosari ikiwemo kifungu kinachoweka kiwango cha adhabu.

“Tuliwahi kukutana na mahakama ambapo mahakimu tuliwaeleza watuambie baadhi ya changamoto wanazopitia katika utendaji wao wa kazi, moja ya changamoto waliyoeleza ni sheria kuwawekea ukomo wa chini wa adhabu jambo linalowapa tabu,” amesema Shangazi.

Kwa upande wake Mbunge wa Kilolo, Justin Nyamoga (CCM) amesema wabunge wataishauri Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, kuangalia namna bora ya kuboresha sheria hiyo ili idumu kwa muda mrefu pamoja na kuimarisha utendaji wa tasnia ya habari.

Mbunge Viti Maalum, Salome Makamba amesema mapendekezo ya wadau yaliyoingizwa katika muswada huo ambayo ni asilimia 35, ni madogo kwa kuwa ilipaswa yafikie asilimia 50 au 60, hivyo wabunge wataishauri kamati hiyo kujumuisha mapendekezo yaliyoachwa.

Awali, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, alisema muswada huo umepunguza adhabu ya kifungo kutoka miaka mitano hadi mitatu, kitendo kitakachopelekea jaji kutoa hukumu ya kifungo kwa mwandishi wa habari, hata kama amefanya kosa linalostahili kifungo cha nje au onyo.

Mjumbe wa Kamati Tendaji ya TEF, Neville Meena, aliwaeleza wabunge hao athari za kifungu cha sheria kinachompa mamlaka waziri mwenye dhamana ya habari kuzuia machapisho kutoka nje, akisema kitendo hicho kinakandamiza uhuru wa habari.

“Katika ulimwengu wa sasa machapisho yapo kwenye mtandao, kuweka Sheria kuzuia machapisho kunalenga dhana ya kuonesha kukabiliana na uhuru wa Habari. Waziri anaweza kukataa kuingizwa gazeti lolote mfano la Kenya ama nchi nyingine kwa sababu tu halitaki kutokana na mambo yake binafsi,” amesema Meena.

Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Huduma za Habari ya 2016, uliwasilishwa bungeni Februari mwaka huu, ambapo wabunge wanatarajiwa kujadili kabla ya kupitishwa kuwa Sheria.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!