Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wabunge Tanzania wanusa ‘madudu’ ujenzi SGR
Habari za Siasa

Wabunge Tanzania wanusa ‘madudu’ ujenzi SGR

Reli ya kisasa ya SGR
Spread the love

 

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu nchini Tanzania, imeonesha wasiwasi wa kukamilika kwa wakati na kwa viwango vya ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande kati ya eneo la Fela Mkoa wa Mwanza hadi Isaka mkoani Shinyanga. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza … (endelea).

Aidha, kamati hiyo imetilia shaka mradi huo wenye loti tano unaotekelezwa na wakandarasi tofauti ambao kukamilika kwake utagharimu zaidi ya Sh.3 trilioni ambao unatarajiwa kukamilika mwaka 2024.

Kamati hiyo ilibaini hayo jana Jumatatu tarehe 14 Machi 2022, ilipotembelea mradi huo kujionea maendeleo ya ujenzi wake.

Mbunge wa Sumbawanga (CCM), Aeshi Hilary hawajaona vifaa vinavyotumika katika ujenzi eneo la mradi na kwamba hali hiyo inaleta wasiwasi kama mkandarasi yuko makini na kazi.

Mbunge huyo aliliomba Shirika la Reli Tanzania (TRC) ambao ni wasimamizi wa ujenzi huo kufanya ufatiliaji wa karibu wa mkandarasi ili kuleta tija katika utekelezaji wa mradi huo.

Naye Mbunge wa Kyela (CCM), Ally Msagila akizungumza katika kikao cha majumuisho ya ziara hiyo, alisema mtu yoyote akiangalia tu kwa macho anaona kazi hairidhishi.

Kwa upande wake, Mbunge wa Singida Mashariki (CCM), Miraji Mtaturu alisema, hajaridhishwa na usalama wa wafanyakazi wa mradi huo kwani baadhi yao wanafanya kazi kwenye mazingira yanayohatarisha usalama wa maisha yao.

Aliwaomba wakandarasi wa mradi huo kuweka vifaa vya usalama kazini katika kila kituo cha wafanyakazi ili kuboresha usalama wao.

Awali, kamati hiyo ilipofika kituo cha Fela walikutana na kundi la wananchi walioweka kambi eneo la Fela, Wilaya ya Misungwi Mkoa wa Mwanza tangu Mei mwaka jana wakisubiri msafara wa kamati hiyo ili kufikisha kilio chao cha kunyimwa ajira.

Akizungumza kwa niaba yao, Paulo Mnema alisema pamoja na wananchi hao kutoka maeneo tofauti nchini kukaa muda mrefu bila kupewa ajira katika mradi huo, kuna urasimu wa kupata ajira zinazotolewa kwani baadhi yao wanaombwa rushwa.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Seleman Kakoso aliitaka wizara ya ujenzi na uchukuzi kufanyia kazi malalamiko hayo ya wananchi na kuangalia hoja zilizotolewa na wabunge.

Aidha, aliwataka wasimamizi wa mradi huo kuwa wazalendo kwa kuangalia maslahi ya wananchi wazawa, kulinda mradi huo usihujumiwe pamoja na kuhakikisha unakamilika kwa wakati.

Naye Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete alisema utekelezaji wa mradi huo kwa sasa umefika asilimia nne na ukitarajiwa kutoa ajira zaidi ya 11,000.

Kuhusu tuhuma za rushwa katika ajira, Mwakibete alisema wizara hiyo itakaa na maofisa rasilimali wa TRC na wakandarasi wanaotekeleza mradi huo ili kumaliza tatizo hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yaanza msako wanaotoa mikopo kausha damu

Spread the loveSERIKALI imeanza kufuatilia watu, vikundi na taasisi zinazotoa kinyume cha...

Habari za Siasa

Spika Tulia aibana Serikali mafao ya wastaafu Jumuiya ya Afrika Mashariki

Spread the loveSPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ameitaka Serikali kufanya tathimini...

Habari za Siasa

Serikali yawapa maagizo Ma-RC udhibiti magonjwa yasiyoambukiza

Spread the loveWAKUU wa mikoa nchini wametakiwa kuandaa utaratibu wa kuwawezesha wananchi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

error: Content is protected !!