Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wa-Ethiopia 24 mbaroni, wengine 23 washikiliwa kwa makosa mengine Mbeya
Habari Mchanganyiko

Wa-Ethiopia 24 mbaroni, wengine 23 washikiliwa kwa makosa mengine Mbeya

Spread the love

JESHI la Polisi mkoani Mbeya, kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama, limewakamata raia 27 wa Ethiopia kwa madai ya kuingia nchini kinyume na taratibu. Anaripoti Keneth Ngelesi, kutoka Mbeya…(endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo, kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Kamishena Msaidizi wa Polisi (ACP), Benjamini Kuzaga, alisema kuwa watuhumiwa walikamatwa katika kijiji cha Igurusi, wilayani Mbarali.

Alisema, walikuwa wakisafirishwa kwenye magari mawili: Moja likiwa na namba ya usajili T 386 DPH, likiwa na tela lenye namba T 939 DGZ na lingine, ni T 410 DPH na tela lenye namba T 574 CNC. Magari yote mawili ni aina ya HOWO.

Kuzaga alisema, wahamiaji wengine sita ambao ni raia wa Ethiopia, walikamatwa katika kata ya Uyole, wakisafirishwa kwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Alisema, wasafirishaji walitumia mbinu ya kuwaficha kwenye kasha la kutunzia vifaa (tools boxes) na kwenye kibini ya gari hizo.

Aidha, mkuu huyo wa polisi wa mkoa amesema, watuhumiwa wengine Mwinyikheri Kitalima, mkazi wa Mwagalisi kwa kukutwa na pembe za ndovu mbili zikiwa na uzito wa kilogramu 42 na kwamba watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kwa tuhuma za uhujumu uchumi.

Katika hatua nyingine, Kuzaga alisema, jeshi hilo linawashilia watu wengine wawili, Mashaka Mtemi na Ubigi Duliya, wakazi wa kijiji cha Mpogolo, wilayani Chunya kwa tuhuma za mauaji.

Watuhumiwa wengine, ni Grace Juma, mkazi wa Kiwila kwa tuhuma za wizi wa mtoto, Amasha Sanga, mkazi wa Ilemi, jijini Mbeya, anayeshikiliwa kwa tuhuma za kusarisha binadamu na watuhumiwa wengine tisa, wanaoshikiliwa kwa kosa na wizi na kuvunja, ikiwamo pikipiki.

Jumla ya watuhumiwa wanaoshikiliwa na polisi, ni 47 wakiwamo hao 24 ambao ni raia wa Ehiopia.

Kutokana na hali hiyo, kamanda Kuzaga ametoa wito kwa watu wote walioibiwa vitu vyao, kufika kituo cha polisi Mbeya.

Naye Kamishna wa Uhamiaji Mkoa wa Mbeya Kigongo Shile alisema kuwa suala la wahamiaji haramu ni changamoto hivyo linapaswa kufanywa kwa kushirikiana na wananchi wote ili kuweza kilitokomeza.

Alisema, serikali haitasita kuwachukulia hatu wale wote wanaojihusisha na usafirishaji wa wahamihaji haramu, huku akiwataka watumishi wa umma hasa vyombo vya ulinzi kujiepusha na biashara hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

error: Content is protected !!