Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Vituo vya huduma kwa jamii vyaanza kutumika Dar
Habari Mchanganyiko

Vituo vya huduma kwa jamii vyaanza kutumika Dar

Spread the love

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imekamilisha ujenzi wa vituo 30 vya huduma kwa jamii (Public Sanitary Service Point) katika wilaya zote tano za Mkoa wa Dar es salaam huku soko la kuku Manzese wakiwa wanufaika wa kwanza tangu kukamilika kwa mradi. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano DAWASA, Everlasting Lyaro ameeleza kuwa vituo hivi vinatajwa kuwa vinara wa usafi wa mazingira na kutoa wito kwa wananchi kulinda miundombinu iliyowekwa kwa matumizi endelevu.

“Vituo hivi vya jamii vinapatikana katika wilaya zote tano ambazo ni Ubungo, Kinondoni, Ilala, Kigamboni na Temeke na vimejengwa katika maeneo yenye mkusanyiko mkubwa wa wananchi hususani katika maeneo ya masoko, stendi za mabasi pamoja na maeneo yenye mikusanyo ya watu wengi kwa lengo la kuboresha usafi wa mazingira kwa wakazi wa maeneo hayo.

“Tumekamilisha mradi wa ujenzi wa vituo 30 kwa ufadhili wa Benki ya Dunia na kwa awamu ya kwanza tumeanza na vyoo vitano na hapa Soko la Kuku Manzese ni wanufaika wa kwanza wa mradi huu na zote ni jitihada zinazofanywa na mamlaka katika kuboresha usafi wa mazingira na kukabiliana na magonjwa ya mlipuko,” amesema Lyaro.

Pia ameeleza kituo cha Manzese kimehusisha matundu ya choo 15 kwa upande wa wanaume na matundu 16 kwa upande wa wanawake, sehemu za kujistiri kwa kina mama pamoja na chumba maalum cha kubadilishia taulo za watoto wadogo na kubwa zaidi ni uwepo wa miundombinu rafiki kwa watu wenye ulemavu.

Naye, Afisa Mtendaji Kata ya Manzese, Rozina Kimario amesema wanaishukuru Serikali kwa utekelezaji wa mradi huu wenye manufaa makubwa kwa jamii hususani wakazi na wafanyabiashara wa eneo hili la Manzese kwani kitaenda kumaliza changamoto iliyokuwepo kwa mda mrefu ya huduma ya choo cha kisasa katika eneo hilo.

Naye Katibu wa wafanyabiashara Soko la Manzese Mustafa Lilonge amesema mradi huo umekuwa msaada kwa wafanyabiashara na kuahidi kutoa ushirikiano kwa DAWASA na kuhimiza usimamizi wa kuvitunza ili kiendelee kutoa huduma endelevu.

“Napenda kutoa shukrani kwa Serikali yangu sikivu kwa kuona umuhimu wa kutuletea wa vyoo hivi, usimamizi mzuri wa manispaa pamoja na uongozi wa Kata ya Manzese.

“Tumeambiwa kituo kinaweza kuhudumia watu zaidi ya 500 kwa siku hii ni kubwa kwetu sio kwamba tulikua hatuna vyoo la hasha vilikuwepo lakini havikuwa bora kilichobaki upande wetu ni kuvitunza na kama kiongozi wa hapa naahidi kutoa ushirikiano kwenye hilo” amesema Lilonge.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!