Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema watinga UN, RPC Dar ampa maelekezo Lissu
Habari za SiasaTangulizi

Chadema watinga UN, RPC Dar ampa maelekezo Lissu

Maandamano Chadema
Spread the love

HATIMAYE Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetinga katika ofisi za Umoja wa Mataifa (UN), jijini Dar es Salaam, baada ya kuandamana Kwa takriban saa tano. Anaripoti Regina Mkonde,Dar es Salaam…(endelea).

Msafara wa Chadema ulioongozwa na viongozi wake waandamizi uliwasili UN majira ya saa 15.10 mchana, tangu ulipoanza saa 10.00 asubuhi katika maeneo ya Buguruni na Mbezi jijini humo.

Baada ya Chadema kuwasili ofisini hapo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, alimpa utaratibu wa kuingia ndani humo, Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu, mbele ya afisa wa UN aliyekuja kuwapokea.

Kamanda Muliro alimweleza Lissu kuwa, kwa mujibu wa itifaki na taratibu za UN, inatakiwa viongozi wanne wa chama hicho akiwemo mwanamke mmoja, waingie ndani kuwasilisha malalamiko yao kisha wakimaliza watatoka nje kuzungumza juu ua kile kilichojiri.

“Mheshimiwa tulikuwa na jambo moja linalofahamika la itifaki, kwa mfumo uliopo wanasisitiza kwamba watu wanne ndio wanaoingia mule akiwemo katibu Mkuu, mwenyekiti Makamu na mwanamke mmoja. Watu wengine watabaki nje watasubiri mambo mengine,” amesema Kamanda Muliro.

Lissu alikubali masharti hayo na kuahidi kwamba Chadema itatekeleza.

“Hatuwezi kuvunja itifaki za UN sisi ni chama cha siasa tunaotekeleza sheria hakuna shaka tutafuata,” amesema Lissu alimweleza afisa wa UN baada ya kupewa maelekezo hayo.

Kwa sasa msafara wa maandamano ya Chadema uko nje ya ofisi hizo wakisubiri kinachoendelea.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!