Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Vita vya Ukraine: Boris Johnson adai kutishiwa kupigwa kombora na Putin
Kimataifa

Vita vya Ukraine: Boris Johnson adai kutishiwa kupigwa kombora na Putin

Boris Johnson, Waziri Mkuu wa Uingereza
Spread the love

ALIYEKUWA Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson amesema, Rais wa Urusi, Vladimir Putin alimtishia kwa shambulizi la kombora katika simu isiyo ya kawaida katika maandalizi ya uvamizi wake, nchini Ukraine.

Waziri mkuu wa wakati huo alisema, Putin alimwambia itachukua dakika moja tu. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Johnson alisema maoni hayo yalitolewa baada ya kuonya kwamba vita dhidi ya Ukraine, vitakuwa “janga kubwa” wakati wa simu “ya muda mrefu” mnamo Februari 2022.

Maelezo ya majibizano hayo yamefichuliwa katika filamu ya BBC, inayochunguza jinsi Putin alivyotangamana na mahusiano yake na na viongozi wa dunia.

Johnson alimuonya Putin kwamba kuivamia Ukraine kutapelekea vikwazo vya Magharibi na wanajeshi zaidi wa Nato kwenye mipaka ya Urusi.

Pia alijaribu kuzuia hatua za kijeshi za Urusi kwa kumwambia Putin kwamba Ukraine haitajiunga na Nato “kwa siku zijazo.”

Lakini Johnson alisema: “Alinitisha wakati mmoja, na akasema, ‘Boris, sitaki kukuumiza, lakini kwa kombora, itachukua dakika moja tu’ au kitu kama hicho.

“Lakini nadhani kutoka kwa sauti tulivu ambayo alikuwa akiitumia aina ya hali yakujitoa hisia ambayo alionekana kuwa nayo, alikuwa akitaka nimshawishi afanye majadiliano.

“Rais Putin alikuwa “amefahamika sana” wakati wa “simu hiyo ya ajabu,” anaeleza Johnson.

Haiwezekani kujua kama tishio la Putin lilikuwa la kweli.

Hata hivyo, kutokana na mashambulizi ya awali ya Urusi dhidi ya Uingereza – huko Salisbury mwaka 2018 – tishio lolote kutoka kwa kiongozi wa Urusi, hata hivyo lilitolewa kwa urahisi, ni sharti lichukuliwe kwa tahadhari.

Lakini wengine wanasema, tishi hilo lililenga kuntishia Johnson ili aweze kulichukua jambo hilo kwa uzito.

Siku tisa baadaye, tarehe 11 Februari, Waziri wa Ulinzi, Ben Wallace alisafiri kwa ndege kwenda Moscow kukutana na mwenzake wa Urusi, Sergei Shoigu.

Makala ya awali ya BBC Putin Vs the West inafichua kuwa Wallace aliondoka na hakikisho kwamba Urusi haitaivamia Ukraine, lakini alisema pande zote mbili zilijua kuwa huo ni uwongo.

Alieleza kuwa ni “kuonyesha uonevu au nguvu, ambayo ni: Nitakudanganya, unajua ninadanganya na najua unajua ninadanganya na bado nitakudanganya.

“Nadhani ilikuwa kuhusu kusema ‘Nina nguvu’,” alisema Wallace.

Alisema “uongo huo wa kutisha, lakini wa moja kwa moja” umethibitisha imani yake kwamba Urusi ingefanya uvamizi dhidi ya jirani yake huyo.

Alipotoka kwenye mkutano, alisema Jenerali Valery Gerasimov – mkuu wa jeshi la Urusi – alimwambia “hatutadhalilishwa tena.”

Chini ya wiki mbili baadaye, vifaru vilipovuka mpaka tarehe 24 Februari, na kwamba Johnson alipokea simu katikati ya usiku kutoka kwa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy.

Alisema, “Zelensky alikuwa ni mtulivu sana,” Johnson alikumbuka.

“Lakini, ananiambia, unajua, wanashambulia kila mahali,” Johnson anasema alijitolea kusaidia kumweka rais kwenye usalama.”

Lakini yeye rais wa Ukraine hakukubali ofa hiyo. Kwa ushujaa alibaki pale alipokuwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!