Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa “Viongozi wa dini ndio wanafanya nchi itawalike”
Habari za Siasa

“Viongozi wa dini ndio wanafanya nchi itawalike”

Askofu Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania na Afrika Mashariki, Emmaus Mwamakula
Spread the love

MCHANGO wa viongozi wa dini katika kuwashauri na kuwasimamia viongozi wa Serikali na kisiasa, ndiyo unaofanya nchi itawalike kwa amani. Anaripoti Mwandishi Wetuy, Dar es Salaam…(endelea).

Hayo yamebainishwa leo tarehe 1 Machi 2024, jijini Dar es Salaam na baadhi ya viongozi wa dini wakihutubia kwenye mkutano wa kuchagua viongozi wa Ngome ya Wazee ya Chama cha ACT-Wazalendo.

Akizungumza katika mkutano huo, Askofu wa Kanisa la Uamsho la Moravian, Emmaus Mwamakula, amesema mara nyingi mambo yanapokuwa hayako sawa, viongozi wa dini hutimiza jukumu lao la kuwaambia ukweli watawala na wapinzani, ili kuweka mambo sawa.

“Tunapokutana na viongozi wenu wa ACT-Wazalendo, Chadema na serikali, kuna mambo ambayo tunayaongea na nhata wakati mwingine tunawekwa kizuizini kwa sababu ya kufanya mazingira ya kuongea na viongozi wote. Kuna mambo ambayo unayafanya kama viongozi wa dini nyuma ya panzia ili kuifanya nchi hii itawalike sababu tunafanya jukumu la kitume la kuifanya nchi itawalike,” amesema Askofu Mwamakula.

 

Katika hatua nyingine, Askofu Mwamakula amesema miaka michache iliyopita nchi ilipitia changamotoi mbalimbali kwenye masuala ya uongozi na utawala bora, lakini kwa sasa mambo yanaanza kubadilika.

Naye Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, amesema viongozi wa dini wana nafasi kubwa katika kuimarisha utulivu wa nchi pale ambapo wanapata nafasi ya kushirikishwa katika masuala ya uongozi.

“Sisi kama viongozi wa dini tuna nafasi yetu kubwa, kwa hivyo pale ambapo mtakapotaka kutushirikisha sisi tunatamka kwamba tuko tayari sababu wale watu ambao ninyi mnataka kuwahudumia sisi ndiyo tuko nao kila siku tunawashirikisha na tunakutana nao mara kwa mara,” amesema Sheikh Ponda.

Kuhusu uchaguzi huo, Sheikh Ponda amewataka wajumbe kuchagua viongozi wazuri watakaosaidia kuwahudumia wanachama wa ACT-Wazalendo na wananchi kwa ujumla.

“Wazee ni watu wa muhimu sana katika jamii yoyote ile kutokana na kwamba ni mtu mzima anakuwa na uzoefu mkubwa wa maisha katika kila eneo, kama ni kwenye biashara, siasa na mambo mengine ya ustawi wa jamii. Mtu mzima anakuwa na uezoefu mkubwa kwa hiyo ni chombo cha kufikiri na fikra ndiyo kitu kinachotengeneza mambo mengine yote,” amesema Sheikh Ponda.

Katika uchaguzi huo, watu wanne wamejitokeza kuwania nafasi ya uenyekiti wa Ngome ya Wazee ya ACT-Wazalendo, ambao ni Mzee Matambara, Mzee Sendwe, Mzee Yasini na Mzee Mapande.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

error: Content is protected !!