Friday , 29 September 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Viongozi Afrika watua Urusi, wateta na Putin
Kimataifa

Viongozi Afrika watua Urusi, wateta na Putin

Spread the love

MKUTANO wa kilele kati ya Urusi na Afrika unaanza leo Alhamisi, ambapo Rais wa nchi hiyo, Vladmir Putin anapanga kuimarisha ushirikiano na mataifa ya Afrika wakati huu nchi yake ikikabiliwa na vikwazo vya kimataifa kwa uvamizi wa Ukraine. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Katika barua yake ya kuwakaribisha washiriki, Putin amesema kuwa ushirikiano wa biashara, uwekezaji, nishati, kupunguza umasikini, kuhakikisha usalama wa chakula na mabadiliko ya tabianchi, vitajadiliwa katika mkutano huo wa kilele.

Putin pia anapanga kukutana na viongozi wa Afrika na kuendeleza mazungumzo kuhusu juhudi za mpango wa amani zinazofanywa na Afrika kwa ajili ya Ukraine.

Imeripotiwa kuwa wawakilishi kutoka nchi 49 kati ya 54 za Afrika watahudhuria mkutano huo unaofanyika St. Petersburg, ambapo 17 ni wakuu wa nchi na serikali.

Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Dmytro Kuleba, anaizuru Liberia, ikiwa ni ziara yake ya tatu barani Afrika tangu Urusi ilipoivamia nchi yake mnamo Februari 2022.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Wadukuzi wa Kichana waiba barua pepe 60,000 za Serikali ya Marekani

Spread the loveWADUKUZI wa kichana wamedukua barua pepe 60000 serikali ya Marekani...

Kimataifa

Mahakama yamkuta na hatia Donald Trump

Spread the love  ALIYEKUWA Rais wa Marekani, Donald Trump, amekutwa na hatia...

Kimataifa

Harusi yageuka msiba 100 wakifariki kwa ajali ya moto

Spread the love  WATU takribani 100, akiwemo bibi na bwana harusi, wamefariki...

Kimataifa

Kampuni ya mali ya China Oceanwide yapata agizo la kufilisiwa huko Bermuda

Spread the love  MAHAKAMA ya Bermuda imetoa amri ya kufilisiwa kwa Kamapuni...

error: Content is protected !!